Mmoja wa Viongozi wakuu wa Kiroho wa Waislam, Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania
Sheikh Hemed Jalala amevitaka Vyombo vya ulinzi nchini pamoja na serikali
kwa ujumla kutambua pamojana kuelewa kuwa vitendo vya ugaidi vinavyotokea nchini
Poamoja na duniani kwa ujumla havina uhusiano wowote na dini ya kiislam kama
jinsi ilivyokaririwa na wengi.
“Makundi mbalimbali kama Al shabab, Bokoharam, Daesh na mengineyo yote
yanayojinasibisha na Uislam, ambao utawakuta wanabeba bendera imeyoandikwa
Laillaha Illa llah, Muhammad Rasulullah, hao sio waislam,kwaniUislam hauruhusu
kumwaga Damu ya Mtu.”amesema Sheikh Jalala
Sheikh Jalala amesema kuwa moja ya sababu ya Ugaidi ni kuwa na fikra ya
Kukufurishana,ambapo inafikia watu wanaitana majina mabaya,na kukufurishana
inamaanakuwa damu yake ni halali,ambapo ni kinyume na mafundisho ya Uislam
ambao aliokujanao Mtume Muhammad (s.a.w.w).
“Dini ya Kiislam sio
dini inayolingania mauaji bali ni dini inayolingania amani,
maelewano,kuvumiliana, kuelewana, kuoneana huruma na mshikamano bila kujali
itikadi za kidini, kikabila, kitaifa na wala kirangi, bali Uislam unalingania
amani kwa watu wote” amesisitiza Sheikh Jalala.
Haya ameyasema leo katika Semina
inayozungumzia Changamoto zinazowakabili Ummah wa Kiislam nchini na
Duniani kwa Ujumla katika Lamada Hotel, ambayo iliyoandaliwa na Taasisi ya
Kiislam ya Imam Bukhar Foundation,chini ya Sheikh Khalifa Khamisi.
Aidha Sheikh amesema kuwa nchi ya Tanzania ni moja kati ya nchi chache
duniani ambazo zinaishi kwa umoja na mshikamano pamoja na upendo wa hali ya juu
hivyo semina hiyo itatumika kuwatahadharisha watanzania kuepuka sana
kukaribisha vitendo vya kigaidi katika nchi yao kwani itasababisha hatari
kubwa.
“Kuwa semina hiyo imekuja mahususi kuwakumbusha waislam jukumu lao la
kujenga umoja miongozi mwao na kwa watanzania kwa ujumla jambo ambalo
litasaidia katika kuendeleza umoja na mshikamano wa watanzania uliopo”.ameongeza
Sheikh Jalala.
Hatahivyo kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Imam Bukhar Foundation
Sheikh Khalifa Khamisi amesema kuwa leo akipatikana mtu mmoja ambaye kavaa
kanzu kafanya vitendo vya kigaidi basi inachukuliwa kuwa waislam woote ni
magaidi dunian,sio kweli na hatufundishi ugaidi katika dini zetu,tunaomba
vyombo vya dola kufuta mawazo haya mabaya juu ya uislam”amesema.
“Kwa sasa waislam
wamekuwa Wahanga kwa kutuhumiwa kuwa wao ndio Magaidi kwa kuwa wanafanya mambo
ya kumkera mwenyezi mungu kwa kuwafanyia wenzao mambo ya maovu jambo aliendani na mafundisho ya Dini ya Uislam ambapo
jambo hili sio kweli bali ni fikra pandikizi zilizopandwa na maadui wa Uislam”amesema
Sheikh Khamisi.
Sheikh Khamis amesema kuwa dini ya kiislam haina mahala popote
inapofundisha watu wake mafunzo ya kigaidi,mauaji,na vitendo vya kinyama
vinavyotendeka duniani hivyo ni lazima watanzania na dunia kwa ujumla kuacha
kuamini kuwa vitendo vya kigaidi vinafanywa na waislam.
No comments:
Post a Comment