Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, hatua ya
hivi karibuni ya jeshi la majini la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu
SEPAH ya kuwakamata wanajeshi wa Marekani walioingia kwenye maji ya Iran
kinyume cha sheria katika Ghuba ya Uajemi, ni kitendo cha kishujaa na
kilichofanyika kwa wakati unaofaa kabisa.
Ayatullah Ali Khamenei amesema hayo leo Jumapili wakati alipoonana na
maafisa wa jeshi la Sepah na sambamba na kuwashukuru wanajeshi hao wa
Iran amesema: Kwa hakika inabidi tulihesabu tukio hilo kuwa limefainyika
kwa taufiki ya Mwenyezi Mungu ambaye aliwafanya wanajeshi wa Marekani
waingie katika maji ya Iran na wanajeshi wetu wachukue hatua ya haraka
na ya kishujaa ya kuwatia mbaroni wanajeshi hao na kuwalazimisha kuweka
mikono vichwani.
Itakukumbukwa kuwa, boti mbili za Marekani, tarehe 12 Januari 2016
zilikamatwa na wanajeshi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu
Sepah baada ya kuingia kinyume cha sheria katika maji ya Iran na kuwatia
mbaroni wanajeshi 10 wa Marekani waliokuwemo kwenye boti hizo.
Wanajeshi hao wa Marekani waliachiliwa huru baada ya kubainika kuwa waliingia kimakosa katika maji ya Iran.chanzo irin
No comments:
Post a Comment