Waislamu wa Nigeria wamefanya maandamano katika miji mbali mbali
ya nchi hiyo kuadhimisha arubaini ya mamia ya ndugu zao waliouawa na
jeshi la nchi hiyo katika mji wa Zaria mwishoni mwa mwaka uliopita.
Maandamano makubwa yameshuhudiwa katika mji wa Kano ambapo
waandamanaji wamelaani mauaji ya mamia ya Waislamu wafuasi wa Harakati
ya Kiislamu Nigeria, huku wakitoa mwito wa kuachiwa huru mwanachuoni wa
Kiislamu nchini humo Sheikh Ibrahim Zakzaky.
Aidha maandamano mengine kama hayo yameshuhudiwa katika miji ya
Sokoto, Minna na Katsina. Hii ni katika hali ambayo, Binti wa Kiongozi
wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amesema kuwa, familia yao haina
taarifa zozote kuhusiana na hatima ya baba na mama yao wanaoshikiliwa na
vikosi vya usalama vya nchi hiyo.
Badia Ibrahim Zakzaky amesema kuwa, baada ya kupita siku arubaini
tangu kutokea maafa ya Zaria ambapo jeshi la Nigeria liliwauwa mamia ya
Waislamu, asasi za kimataifa zimeshindwa kuandaa mazingira ya yeye
kukutana na baba na mama yake wanaoshikiliwa na vikosi vya usalama vya
Nigeria.
Itakumbukwa kuwa, mwezi Disemba mwaka jana, wanajeshi wa Nigeria
waliwavamia Waislamu wa mji wa Zaria, kaskazini mwa nchi hiyo na kuwaua
kwa umati mamia ya Waislamu.
Vilevile walimpiga risasi kadhaa na baadaye kumkamata Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo.chanzo irib
No comments:
Post a Comment