Kahtibu wa Swala ya Ijumaa, Sheikh Ramadhani Kwezi, Jana Masjid Bilal Temeke, Dar es salaam. |
Khatbu wa Swala ya Ijumaa Sheikh Ramadhani Kwezi amewataka
Waislamu watanzania kujitolea nafsi zao kwa hali na mali katika kuhakikisha
kuueneza na kuulinda Mila na Desturi na mafundisho ya Dini tukufu ya Uislamu.
Sheikh Kwezi alisema hayo jana katika Khutba ya
Swala ya Ijumaa, iliyoswaliwa Masjid Bilal Temeke, Jijini Dar es salaam,
akizungumzia Mazazi ya Bibi Zainabu bint Ali (a.s) na kusema Bibi Zainab
aliitoa Nafsi yake katika Kulinda Dini tukufu ya Uislamu.
Sheikh Kwezi alisema kuwa Uislamu umewakataza Waislamu
kufanya Matendo, Vitendo na mambo yote ambayo ni mabaya hayana maslahi katika
Jamii, hayana maslahi kwa mtu mmja mmoja, na mambo amabyo yanavuruga na
kusambaratisha Umma wa Kiislamu.
“Matendo,Vitendo na mambo mbalimbali au shughuli mbalimbali
ambazo ni mbaya hazina maslahi kwa Umma,hazina mashalahi kwa mtu mmoja mmoja
wala kwa jamii,bali ni mambo ambayo yanavuruga na kusambaratisha Umma wa
Kiislamu Tumekatazwa” alisema Sheikh Kwezi.
Aidha Sheikh Kwezi amewataka Waislamu na Watanzania
kuhakikisha wanafanya Uadilifu, Ihsani na Kutoa Sadaka na kutokuwadhulumu watu na
kusema kuwa kufanya hivyo ni kufuata mafundisho na maamrisho ya Mwenyezi Mungu ambae
ni muumba wa Vitu vyote Ulimwenguni.
Mwenyezi Mungu anasema “Hakika Mwenyezi Mungu anatuamrusha
tuishi kwa Uadilifu yaani kila mtu apewe anachostahiki, kwa Ihsani yaani
Matendo mema, kufanyiana wenyewe kwa wenyewe mambo mazuri, kuwasaidia
mayatima,Wajane na wenyeshida na kutoa kwa watu wa karibu”
Hatahivyo Sheikh Kwezi amewataka Waislamu na Watanzania
kumuiga na kumfuta Bibi Zainabu (a.s) katika Ushujaa na Ujasiri na kusimama
imara katika kuhakikisha haki inatengeka, Uadilifu unafanyika, Dhulma
haitakiwa, Mambo mabaya hayatakiwi, na maonevu hayatakiwi.
Bibi Zainabu (a.s) ni Mmoja katika Mashujaa wa Karbala,
aliesimama Imara katika ardhi ya Karbala nchini Iraq,Bibi zainabu ni mmoja kati
ya wale amabo wanadaraja kubwa sana mbele ya Mwenyezi Mungu (swt), Bibi Zainabu
Baba yake ni Sayyidna Ali Ibn Abutwalib
(a.s) na Mama yake ni Fatuma Bint Muhammad (a.s). Bibi Zainabu alizaliwa tarehe
5 Jumadal al Awal mwaka wa 5 AH sawa na tarehe 2, Oktoba mwaka wa 625 AD.
No comments:
Post a Comment