Kiongozi
Mkuu wa Waislamu dhehebu la shia Ithnasheria Tanazaia Sheikh Hemed Jalala amesema Walemavu wa Ngozi ni Binaadam kama binaadam wengine (Watanzania), kwani binadam ni kiumbe kitukufu mbele ya Mwenyezimungu.
"jamii ifahamu kuwa
hakuna njia ya mkato ya kupata utajiri na kwamba wale wote ambao wanaamini
katika kuua watu wenye ulemavu wa ngozi ili wanufaike wanapaswa kuacha tabia
hiyo kwani ni kwenda kinyume na mufundisho ya dini zote duniani"...
"Wito kwa Watanzania kupinga mauaji ya Albino kwa vitendo na kuwataka viongozi
wa dini kutumia membari zao kukemea viitendo viovu vya mauaji ya albino"amesisitiza Sheikh Jalala
Akizungumza
katika iftari maalum na watu wenye ulemavu wa ngozi kutoka Wilaya ya Kinondoni,
hapa Masjid Ghadir, Kigogo-Post Dar es salaam, Sheikh Jalala amesema viongozi wa dini na Watanzania kwa ujumla wanapaswa
kulizungumza hilo bila woga kwani hiyo ndiyo njia pekee ya kuwasaidia watu
wenye ulemavu wa ngozi.
Amesema
Albino ni binadamu kama walivyo watu wengine hapa nchini, wanahaki sawa ya
kuishi, kulindwa na nyinginezo hivyo si haki kukatiza maisha ya watu hao na
kwamba dini zote za duniani haziruhusu watu kuuana.
Aidha
sheikh Jalala amefafanua njia nzuri za kupata utajiri kuwa ni kufanya kazi kwa
bidii zote na si kuwaza Imaani potofu ya kuua watu wengine ambao hawana hatia.
Amesema
kitendo cha kuua kinazima ndoto zao, hivyo ni wakati watu wakafahamu hilo na
kuachana na tabia hiyo ambayo inatia doa Taifa la Tanzania huko Ulimwenguni.
“Nataka
niseme, tendo la kuwaita wenzetu wenye ulemavu wa ngozi na kushiriki pamoja
futari ya jioni hii ni kuonyesha kuwa hawa ni wenzetu, hawana utofauti wowote
na wengine, wanahaki sawa kama Watanzania…kuwaua ni matendo ya kishetani na
hayakubariki” alisema Sheikh Jalala.
Amesema
wale wote ambao bado wana Imaani ya kuua ili watajirike ni washamba na hawajui
walifanyalo, wanapaswa kufahamu kuwa utajiri hauletwi kwa damu za watu badala
yake ni kujituma kwa kufanya kazi inayompendeza Mungu.
Katika
hatua nyingine Sheikh Jalala amewaahidi chama cha watu wenye ulemavu wa Ngozi
Wilaya ya Kinondoni kuwapa ushirikiano wowote watakaouhitaji na kwamba
wanakaribishwa katika msikiti wa Kigogo
muda wowote na watapewa ushirikiano unaostahili.
“Nataka
niwaambie ndugu zangu wenye ulemavu wa ngozi hapa Tanzania sisi hapa Kigogo
tunawapenda na tunawakaribisha hapa msikitini ,sisi hatujui kubaguana,muone
kama mko nyumbani na kwamba muda wowote mkiwa na haja ya kutuona milango iko
wazi na mnakaribishwa sana ”Alisema Sheikh Jalala.
Akizungumzia
Msikiti wa Kigogo Sheikh Jalala amesema ni kimbilio la watu wote, ni msikiti wa
wakristo, watu wenye ulemavu wa ngozi, wajane na masikini. Ni msikiti ambao
unajari imaani za watu tofauti kwani wanaamini kuwa haitokea siku moja nchi
yote ya Tanzania kukawa na dini moja hivyo si wakati wa kubaguwana.
Haitakaa
itokee Tanzania kukawa na dini moja mpaka dunia inapogota mwisho wake…lakini
mtakubaliana na mimi kuwa Mungu aliyeumba Mkiristu ndiyo huyo aliyemuumba
muislamu na wale wa Dini nyingine, Mwanzo wa binadamu ni uleule wa Adamu na
hawa…tofauti zilizopo ni za kibinadamu hatuna haja ya kubaguana.Alisema.
No comments:
Post a Comment