Friday, March 11, 2016

SIMAMIENI SHERIA NA TARATIBU KWA UADILIFU MKUBWA – KAIRUKI

pi1Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki  amewataka Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu kusimamia Sheria na Kanuni kwa uadilifu na kutoa fursa sawa kwa watumishi ili kuleta tija na ufanisi katika maeneo yao ya kazi.Mhe. Waziri alisema hayo alipokuwa akifungua mafunzo ya maadili kwa makatibu wakuu na Manaibu katibu wakuu yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam.
 
Amewataka viongozi hao pia kuendesha shughuli zao kwa kushirikisha watendaji wanao wanaongoaza na kuachana na tabia za upendeleo ili kufanya kaingira ya kaazi yanakuwa bora na yenye kuleta ufanisi.

“Muwe na uongozi shirikishi , mtende haki na msimamie Sheria na Taratibu na kuacha tabia za kufanya maamuzi kwa upendeleo kwani kufanya hivyo kutafanya kuwe na mazingira bora ya utendaji kazi ndani ya Serikali”, alisema Mhe. Kairuki

Amesema wao kama viongozi wakifanya na kuzingatia hayo watakuwa wametekeleza majukumu yao kwa mujibu wa Sheria na hivyo kuwa na utendaji uliotukuka.
pi1
Aidha amezitaka Wizara na Idara za Serikali kuanzisha vitabu vitakavyosajili zawadi ambazo viongozi na watumishi wa umma wanapewa wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao ili kuwa na usimamizi mzuri wa suala hilo.

 Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma inawataka Viongoai kukabidhi zawadi wanazopewa wanapotekeleza majukumu yao zenye thamani ya zaidi ya sh 50,000 kwa maafisa masuuli wao ili kuepuka mgongano wa maslahi

Awali akizungumza katika mafunzo hayo Katibu Mkuu Kiongozi mhe. Balozi John Kijazi aliwasisitizia watendaji hao wakuu wa Serikali kusimamia maadili ili kufaniksiha utendaji uliotukuka ndani ya Serikali.

Amesema lengo la Serikali ya awamu ya tano ni kuwaleteae maendeleo ya kweli wananchi kwa kuwaondolea umasikini na kusisistiza kama wote walivyotia saini Hati ya Ahadi ya Uadilifu siku waliyoapishwa ni wajibu wao kuhakikisha wanaishi kwa mujibu wa viapo hivyo.

Aliwataka Makatibu wakuu na Manaibu hao kuhakikisha wanasimamia sheria na taratibu zilizotolewa na Serikali na ni imani yake kuwa watasimamia hiyo kama walivyoapa,

No comments: