Serikali ya Uganda imepuuza vikwazo ilivyowekewa na
serikali ya Marekani kutokana na kupitisha sheria ya kupiga marufuku ndoa za
watu wa jinsia moja. Ofwono Oppondo, msemaji wa serikali ya Uganda amesema
kuwa, vikwazo vya Washington dhidi ya nchi yake, vitakuwa na taathira ndogo tu
kwa uchumi wa Uganda.
Ofwono pia amekadhibisha tuhuma zisizo na msingi
zilizotolewa na Marekani kwamba vitendo vya ukatili na ukandamizaji dhidi ya
watu wa jinsia moja wanaojamiana hasa baada ya kupitishwa sheria ya kupiga
marufuku vitendo hivyo vichafu vimeongezea nchini Uganda na kusema kuwa, madai
hayo ni ya kipuuzi. Amesisitiza kuwa, kuanzia sasa Waganda watajidhaminia
wenyewe mahitaji hayo na hawatakubali kufanywa watumwa wa wafadhili.
Sheria ya kupiga marufuku liwati na usagaji nchini
Uganda ilipasishwa mwezi Februari mwaka huu. Hata hivyo madola ya Magharibi
kama vile Denmark, Norway, Uholanzi, Sweden na Marekani zilipinga vikali hatua
hiyo.
Juzi Marekani ilipasisha muswada wa kuiwekea vikwazo
serikali ya Kampala na kukata misaada yake ya kifedha kwa nchi hiyo. irib
No comments:
Post a Comment