Meneja wa Hawza ya Imam Jafar Swadiq Chini ya Sheikh Hemed Jalala, amewataka watu kutoa misaada ya hali na mali kwa watu wanaoishi Magerezani kwa kuzingatia wao ni Binaadam wanahitaji mahitaji kama watu walio huru.
Hayo yamesemwa leo na Sheikh Salim Mwamba wakati walipotembelea
Mahabusu ya Watoto, Upanga Jijini Dar es salaam, wakikumbuka kifo cha Mjukuu wa
Mtume Imam Hussein (a.s).
“Sio kila aliye Gerezani ni
mkosa,kwani wao wanahitaji huduma za kijamii kama chakula na mavazi kama watu
walio huru” alisema sheikh Mwamba.
“Imam Hassan Askari na Nabii Yusuph walifungwa Gerezani na hali ya
kuwa hawana makosa”ameongeza Sheikh Mwamba.
Sheikh Mwamba amewataka askari magereza kuwa na moyo wa ubinaadam,
kwa kuwatendea Haki na Uadilifu wafungwa waliopo gerezani kwa kuwa ni watu kama
wao na wanamahitaji kama yao.
Wanaharakati wa Imam Jafar Swadiq wanafanya shughuli mbalimbali za
kijamii kama Kusafisha Makaburi, Kutembelea magereza, kusafisha barabara na
kujitoea damu, kwa ajili ya kuadhimisha kifo cha Mjukuu wa Mtume Muhammad
(s.a.w.w) ambaye ni Imam Hussein ibn Ali.
Imam Hussein (a.s) alizaliwa tarehe 15, mwezi wa Shaaban Mwaka 4
A.H na Fatma bint wa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Amirul Muuminina Ally
na aliuwawa tarehe 10 Muharram katika mji wa karbala nchini Iraq.
No comments:
Post a Comment