Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania amesema kuwa,
Tanzania ni lango la kuingizia bidhaa za Kiirani katika eneo la Afrika
Mashariki.
Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran nchini Tanzania Mehdi Agha Ja'fari |
Balozi Mehdi Agha Ja'fari amezungumzia uwanja wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusema kuwa, katika miaka ya hivi karibuni, Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi muhimu mno kwa ajili ya kusafirisha na kupeleka nje bidhaa za Iran zisizo za mafuta na hivyo kuifanya nchi hiyo kuwa lango la kuingiza bidhaa za Kiirani huko Afrika Mashariki.
Balozi Mehdi Agha Ja'fari amesema, Tanzania na bandari ya Dar es Salaam kuwa pambizoni mwa bahari ya Hindi na kuwa kwake karibu na maeneo ya kiuchumi ya magharibi mwa Asia hususan Ghuba ya Uajemi ni sifa nzuri zinazotayarisha mazingira bora ya kufanyika biashara kati ya Tanzania na Iran.
Balozi wa Iran mjini Dar es Salaam amesema kuwa, takwimu
zinaonyesha kuwa, usafirishaji wa bidhaa zisizo za mafuta za Iran
kuelekea Tanzania umeongezeka mno katika kipindi cha miaka minne ya hivi
karibuni. Chanzo cha habari:
chanzo Afroshia
Taasisi ya Bilal Muslim Mission ya Tanzania inaungana pamoja na watafuta haki na usawa wote duniani kuonesha mshtuko wao kwa hukumu ya kifo iliyotolewa kwa Sheikh Nimr Baqr Al-Nimr kwa madai yake ya kutaka haki na usawa kwa wananchi nchini Saudi Arabia
Tunaomba muungano wa wapenda haki na usawa duniani kote kuitaka mamlaka ya nchini Saudi Arabia kufuta hukumu ya kifo kwa Sheikh Al-Nimr. Na kuwa serikali nchini humo imuachie kwa moyo wa kidemokrasia, maadili na kanuni kama zilizoanishwa katika tangazo la haki za binaadamu la Umoja wa Mataifa.
Kusiwe na Taifa katika Umoja wa Mataifa ambalo litajiwekea utawala wa kisiasa ambao si wa Jamhuri ya kidemokrasia. Vinginevyo ni uvunjwaji wa haki za binaadamu.
Asibughudhiwe mtu kwa kusimama kwake na kutete haki za binaadamu kwa kiasi cha uhuru wake wa kidemokrasia, kujitegemea na usawa wa watu na haki zao.
Binadamu wawe ni familia moja katika kuhifadhi haki ya utu wao, Haki ya uhuru wa kujieleza, Haki ya Kidemokrasia, Matakwa binafsi na Utawala wa kujitegemea.
- See more at: http://www.dunialeo.com/sw/posts/browse/local-news/bilal-muslim-mission-ya-tanzania-yalaani-hukumu-ya-kifo-kwa-shk-nimr-1#sthash.M7BGl1Aw.dpuf

No comments:
Post a Comment