Saturday, September 19, 2015

Vijana watakiwa kuwa makini na wagombea katika Uchaguzi Mkuu


Naibu Imam wa Masjid Ghadir Shiekh Ghawth Nyambwa amewataka Vijana kuwa makini na Wagombea ambao ni waongo wasio kuwaa na maadili wenye chuki za kidini, kimadhehebu na kikanda.Haya ameyasema leo katika Khutba ya Swala ya Ijumaa, iMasjid Ghadir, Kigogp Post, Dar es salaam na kusema kuwa Maadui wakubwa wa Waislam na Wapenda haki ni Wamarekani na Waizrael ambao nchi nyingi za Arab na Afrika wao ndio wachochezi wa Vurugu zinazoendelea Duniani.
Aidha amesema kuwa Siku za hijja ni siku za Waislam Dunian na ni moja ya njia kuu ya kutatua matatizo ya magonjwa, umasikini, kukosa elimu, vita duniani, machafuko ya kisiasa, na chuki za kidini na madhehebu.
"Kama malengo ya hija yakitumika vizuri, hija itaweza kutatua matatizo ya waislam, watatatua matatizo yote ulimwenguni."amesema sheikh nyambwa.
Sheikh Nyambwa amewataka wanasiasa kuwa wakweli na kuheshimiana katika kamepeni zao na kutimiza ahadi wanazoziahidi ziwe ahadi zinazotekelezeka.
" watanzania kumchagua kiongozi ambae ni Muadilifu na mwenye Sera nzuri zinatakazo dumisha amani na ushirikano baina ya watanzania."amesema sheikh nyambwa.
Hatahivyo Sheikh Nyambwa amesema Moja ya mafundisho na falasafa ya hijja ni Kulingania amani na maelewano baina ya watu wote, na kuwataka Waislam pamoja na Watanzania kuiombea taiga letu suala la kudumisha amani hususan kipindi hiki cha Uchaguzi wa Raisi, Ubunge na Udiwani

No comments: