Sheria ya mwaka 1977, ibara ya 74,kifungo kidogo cha
6 (b),inaipa tume ya uchaguzi mamlaka ya kisimamia na kuratibu uendeshaji uchaguzi wa Raisi, Ubunge
na Udiwani.
Pili uchaguzi wa uraisi wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania unasimamiwa na Tume ya Uchaguzi ni tofauti na uchaguzi wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar .hii ni kwa sababu tume hizi zinasimamiwa na
Katiba na Sheria tofauti.
Tatu uchaguzi wa Zanzibar unasimamiwa na katiba na sheria ya
Zanzibar ya mwaka wa 1984, ya uchaguzi
wa Jamhuri ya Muungano inasimamiwa na katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka
1977.
Nne, Ibara ya 38, kifungu kidogo cha katiba ya
Jamhuri ya Muungano inaelezwa kuwa Raisi atachaguliwa na Wananchi kwamujibu wa
Masharti ya katiba na kwa mujibu wa sheria itakayoweka
masharti,kuhusu uchaguzi wa Raisi ambapo
itatungwa na bunge la Jamhuri ya Muungano.
Tano Ibara ya 104, kifungu kidogo cha katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema, kuwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Serikali ya
Zanzibar atachaguliwa na Wananchi wa
Tanzania Zanzibar kwa mujibu wa masharti
ya katiba ya Zanzibar na kwa kufuata
utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria uliyotungwa na Baraza la Wawakilishi la
Zanzibar inayohusu Uchaguzi kwa Ujumla na uchaguzi Kiongozi wa Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar
Sita, Sheria ya Uchaguzi ya sura ya 343, inaweka
masharti ya uchaguzi wa Raisi ,Wabunge na Udiwani wa Jamhuri ya Muungano .
Saba, Tume ya Uchaguzi katika kutekeleza masharti ya
sheria ya Taifa ya Uchaguzi ambayo
inasimamia uchaguzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka Vituo
vya kupigia na kuhesabu kura, daftari kwa kila kituo,masanduku ya
kupigia kura na fomu mbalimbali ambayo
ni tofauti na Tume ya Uchaguzi wa
Zanzibar
Nane, pmoja na Hilo tume ya Taifa ya Uchaguzi , kwa
upande wa Uchaguzi wa Kura za Uraisi na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano, Zanzibar kuteuliwa na kuweka mtendaji wake
ambao watatoa taarifa wa uchaguzi moja kwa noja kwa tume na sio kwa ZEC .
Tisa,katika zoezi la upigaji kura pamoja na
kupandika kura ya raisi , na wabunge wa Jamhuri ya Muungano upande wa Zanzibar ,Tume
ya Taifa ya Uchaguzi , kusimamia yenyewe
mchakato wote huu .
Kumi, Hadi sasa Tume imeshapokea matokeo ya kura za Uraisi kutoka majimbo yote
ya Zanzibar na imeshayatangaza .
Kumi na Moja, Hakuna taarifa zozote za dosari kuhusu
mchakato wa Upigaji kura za Uraisi,Ubunge na Udiwani wa Jamhuri ya Muungano
kutoka Zanzibar ambazo zimepokelew.
Kumi na Mbili, kwa maana hiyo basi tume ya taifa ya
uchaguzi inapenda kuwaarifu Watanzania
wote kuwa mchakato wa Uchaguzi wa Uraisi
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Unaendelea
kama kawaida iliyokuwa imepangwa.
Kumi na Tatu, taarifa za Uvumi,kuwa Uchaguzi wa
Jamhuri ya Muungamo kuwa Umefutwa hiyo si kweli, ni Uvumi, ni Uongo na
Upotoshaji na sio taarifa sahihi na zinapaswa kupuuzwa na sasa tunaendelea
na utangazaji wa Matokeo ya Awali kama
kawaida .chanzo radio one
No comments:
Post a Comment