Mmoja wa Viongozi wakuu
wa Kiroho wa waislam, dhehebu la shia Ithnasheriya Tanzania amesema Watanzania
walikuwa hawana sifa wala tabia ya kuitana huyu sunu, huyu shia, Yule Mkristo Yule
Muislam,bali walikuwa wanaitana kwa jina la Utanzania na walikuwa hawana tabia
ya ubaguzi wa dini.
Sheikh Jalala amesema
kwa kuwa kwa utulivu tuliokuwa nao tayari maadui wanatengeneza mbegu mbaya na
kuziingiza ndani ya nchi, ili kuharibu hali hii tuliyokuwa nayo yupo adui
anataka kutengeneza ya kwamba hawa ni Madhehebu hii, wale ni madhehebu ile nah
ii ni hatari katika uslama wan chi hii ya Tanzania.
Aidha Sheikh Jalala amevihatarisha Vyombo vya Uslama kuwa
makini mmo, na kutowanyamazia watu hao, kwa sababu wanaotesha nyama mbaya na ni nyama hatari sana kwa mstakabali wan
chi kama ya Tanzania inayojulikana kama kisiwa cha amani na utulivu.
Sheikh Jalala amesema haya
katika Khutba ya Swala ya Ijumaa Masjd
Ghadir, Kigogogo-Post,Dar es salaam na kusema kuwa watanzania hawajui ubaguzi
wa dini, na sisi ni watanzania Wakiristo na waislam wanaishi kwa pamoja bila
itikadi zozote hatari za Dini, ukabila wala rangi.
“Tanzania inasifika kuwa
kisiwa cha amani,leo maadui wote wa Tanzania wanakimbilia Tanzania kuja
kutengeneza magurupo ya Kukufurishana, Ubaguzi wa Dini, Rangi na ndio wanakuja
kuharibu utulivu huu tuliokuwa nao” amesema Sheikh Jalala.
Sheikh Jalala
amesisitiza kuwa Tanzania ni kisiwa cha amani, Tanzania tunamawahusiano mazuri
na madhehebu zote pamoja na dini zote, hakuna ubaguzi hapa kati ya Ushia na
Usuni au Uislam na Ukristo, Wakristo, Waislam, Mashia , masuni tunakaa meza
moja kwenye vikao vya amani na maelewano na haya hayapo katika baadhi ya nchi.
No comments:
Post a Comment