Kingunge amevua rasmi uanachama wa CCM na amesema sababu ya kujitoa CCM
ni kutoridhishwa na mwenendo wa chama hicho kwasasa na hatojiunga na
chama kingine ila yuko upande wa mabadiliko
Kingunge- "Kila
unapopita vijana,kinamama, na watanzania wote wanataka mabadiliko na
mimi niko upande wa mabadiliko na yaje haraka"
Kingunge- "Wanabadilisha kibwagizwo toka kidumu 'chama cha mapinduzi'
hadi 'kidumu chama tawala', hapo ni kung'ang'ania madaraka"
Kingunge- "Baada ya kukaa madarakani muda mrefu chama cha CCM hakiwezi kufanya jipya, chama kikikaa nusu karne hakina jipya tena"
Kingunge- "Mabadiliko ni muhimu kweli kweli, upate watu wengine wenye pumzi mpya, mnataka mbakie nyinyi tu, nyie pumzi imekwisha"
Kingunge -" Sisemi chama hiki cha zamani kisifanye kazi, kiwekwe kando kwa muda, CCM imeacha kujadili issues sijui wanajadili nini"
Kingunge- "Wanaotaka tuondoke hapa twende mbele lazima watu wapya waongoze, lazima fikra mpya ziongoze".
Kingunge- "Tumefika mahali pagumu sana, nguvu ya kupinga mabadiliko ni kubwa ila kwa utafiti wangu nguvu ya wanaotaka mabadiliko ni kubwa zaidi hivyo msiogope" amemalizia kwa kusema hayo

No comments:
Post a Comment