Mmoja wa Viongozi Wakuu wa Kiroho wa Waislam, Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala, akiongea na Wanahabari juu ya Chanzo cha Vifo vya Mahujaji, punde tu baada ya kutoka Hijja |
Bismillah
Rahmani Rahim.
Asalam
Alaykum Warahmatullah Wabarakatu
Ujumbe
wa Sheikh Hemed Jalala baada tu ya Kurejea kutoka katika Ibada ya Hijja, 16 Dhulhijja
1436, Sawa na 30/09/2015
Kwa kuwa kama mtanzania
na mmoja katika viongozi wakuu wa kiroho wa waislam,dhehebu la shia
Ithnasheriya Tanzania na kwa kuwa leo ndio tumefika katika miongoni mwa
misafari inayotoka Hijja.
Nadhania itakuwa vizuri zaidi na mimi nishiriki
pamoja na watanzania wenzangu, ambao bila shaka wanashauku kubwa na wanahamu
kubwa yakutaka kujua yaliyotokea katika ardhi takatifu.
Nipende kusema
kwamba tunamshukuru Mungu (swt) tumemaliza
ibada hii ya hijja kwa usalama sisi kama watanzania, lakini jambo la
kusikitisha na la kuliza kwamba hatukurudi sote salama ambao tuliokwenda
kutekeleza hiyo ibada ya hijja, wako ndugu zetu ambao badala ya kuwapokea
mahujaji wao,wamepokea habari za kusikitisha, habari za kilio na habari za
msiba.
Napenda kwa kweli kuwapa
pole wote watanzania ambao waliokumbwa na msiba huu kwa nyumba zote ambazo watu wake wamefariki katika
ardhi ya minna, mwenyezimungu (swt) watu hao awape shubira awape uvumilivu,na
awalipe kila la kheri, vilevile kwa msiba huu uliowatokea, na ninaamini ni
msiba wa Kitaifa na Kimataifa kwa watanzania wote.
Baada ya kusema hayo
niseme kwakweli pamoja ya kwamba tumetekeleza ibada yetu hii ya hijja kwa
salama,lakini naweza kusema kwa kweli kilichotokea katika ibada ya mwaka huu ni jambo la
kutisha na ni jambo la kusikitisha na ni
jambo ambalo kunyamaziwa kimya kwa kweli sio sawasawa na sio mahala pake.Idadi
ya watu waliokufa ni wengi mno, na tukizungumza ripoti ya mwisho mwishoidadi isiopungua zaidi ya Mahujaji 4000
Na hawa wamepotea na
tunaposema wamepotea la siwezi kusema ninaudhibitisho kuwa wamekufa ,lakini
wamepotea wapi? Tunapozungumza Minna ni mtaa na vilevile tunazungumza sio kama
watu wamefunikwa na kifusi, hapana, bali ni watu walio kufa njiani, kwahivyo
tumewakosa watu hawa, watu 4000 ni watu wengi mno,hakuna taifa ambalo halijaguswa
na msiba huu
Je,kutokea jambo hili
katika zama hizi ni mahala pake? Ukiliangalia tukio la kumpiga shetani siku ya
Eid, vikuta hivi ni vikuta vikubwa wapo watu wanapiga chini na wengine juu na
baada ya kupiga watu wanatoka na hawarudi, lakini kwanini hili limetokea. Hili
limetokea kwa sababu hizi njia kuu zilifungwa, njia ambzo ndio kuu zilifungwa,
kwani njia hizi kuu zingiwa wazi, lisingetokea tukio lolote.
Na ndio maana tunaona
kwamba sehemu za kupiga shetani kutoka zimepanuliwa haijawahi kutokea tukio la
vifo katika sehemu hizo, kwahivyo kilichotokea ni kwamba sehemu hizi zilifungwa
mahujaji pamoja na wingi wao wakatakiwa wapite katika njia ambazo sio njia pana
hapa wakakusanyika wanaokuja kumpiga shetani na wanaorudi kutoka kumpiga
shetani, pakatokea maafa ya kusikitisha.
Sisi na nikiwemo mimi
kama Imam wa Msikiti wa Ghadir, Kigogo-Post, na Mmoja wa Viongozi wa Wakuu wa
Waislama, Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania kwa kweli ninaibebesha Serekali
ya Saudia Arabia kwa Uzembe uliotendeka na uliofanyika katika tukio hili.
Serikali ya Kifalme ya Saudia Arabia inabeba dhima hii kubwa, kwanini
inabeba,inabeba kwa sababu kwanza zipo barabara kubwa ambazo hazipungui mita
30,
kwa nini mahujaji wasiruhusiwe
kupita barabara hizo, hili la kwanza , la pili na hili ni muhimu vilevile la
kuliangalia kwa makini sehemu takatifu zimezungukwa na Kamera , hivi hizi
kamera hazikuona watu wanokufa,kwani kila baada ya dakika 3 walikuwa wanakufa watu
wasiopungua watano.
Kwa hiyo mimi naamini
na ni msimamo wangu kwamba serikali ya Saudia Arabia inabeba jukumu lote la
kutokea vifo vya mahujaji hawa, kama inavyobeba jukumu la kizembe la kwanza
lililotokea katika ardhi ya makka lililotokea katika msikiti, masjid Haram,
swala la Winchi,hili linabeba serikali na Serikali yenyewe imekubali kwamba ni kosa
imefanya.
Lakufanya ni nini? Kama
watanzania mimi ningeiomba serikali na viongozi wa nchi watambue ya kwamba
tunapokwenda hijja hatwendi kufa, tunakwnda kutekeleza moja ya nguzo za
Kiislam, kwahiyo hatwendi kule kufa, hiyo ieleweke,na kama kuna watu
wanaitikadi hiyo, itikadi hiyo sio sawasawa.
Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ni lazima iungane na nchi ambazo zinaidadi kubwa ya
Mahujaji inayowapeleka serikali iungane nao katika kuhakikisha kwamba
wanashirikishwa katika upangaji wa Ibada ya Hijja. Kushiriki katika kupanga
Ibada ya hijja haina maana tumeingilia mamlaka ya Serikali ya Saudia Arabia ,haina
maana hiyo.kwa sababu Ibada ya hijja ni Ibada ya Waislam wote. Ili nayo ione na
ikinaike, Je, inayohaki kuwapeleka watanzania katika ibada hiyo wakaenda na wakurudi
salama. Hili ni jambo la kwanza serikali inaweza kulifanya.
Jambo la pili ambalo
linaweza kufanyika ni zile nchi za Kiislam (OIC) ni umoja wa Nchi za
Kiislam,umoja huu usimamie, kwa sababu taratibu zote zinaonesha kwamba serikali
ya Saudia Arabia imefeli katika kupanga Ibada ya hija ndio yakatokea mauaji
haya ya Kimbari.kwa hivyo umoja wa nchi za Kiislam zilisimamie Ibada hii ili
iende salama.
Na kwa kuwa hija ni
Ibada ya Usalama, ibada ya maelewano ni Ibada ya Amani na muanzilishi mkuu wa
ibada hii ni Nabii Ibrahim (a.s), Nabii Ibrahim ni Nabii wa watu wote , ni
Nabii wa Waislam, ni Nabii wa Wakristo, Ibrahim(a.s) alimzaa Ishaq (a.s) ni
mtume anaekubalika kwa ndugu zetu Wakristo na Ismail (a.s) ni mtume
anaekubalika kwa Waislam na Wakristo.
Niseme kwamba Ibada hii
sisi mahujaji tunauombea mungu Uchaguzi ambao ndio tupo karibuni kuingia.
Tunaiombea sisi kama Mahujaji mimi na wenzangu tumeorudi katika msafara huu
kwamba Mungu aibakishe amani na utulivu na maelewano nchi hii katika kipindi
hiki kigumu ambacho tunaingia, Niliwahi kuongea na ninaendelea kuongea yakwamba
miongoni mwa Vigezo vikubwa vya kura zetu tumpe nani,
Tumpe Yule mtu ambaye
anawataka watanzania kuwa kitu kimoja , anawataka watanzania wawe ndugu, yeyote
ambae mantiki yake , fikra zake ni kuwagawanya Waislam na Wakristo kuwagawanya
watu wenye dini tofauti ambao wanaokaa vizuri, huyu ndugu zangu Watanzania
hatuna haki ya kumpa kura zetu. Mungu aibariki Tanzania, Mungu aupitishe
Uchaguzi huu uwe Huru, Uwe Salalama na Tanzania ibakie kuwa nchi ya amani,
Utulivu, Maelewano na Busara.
Asanteni
Sana
Wabillah
Tawfiq
No comments:
Post a Comment