Kiongozi
Mkuu wa Chuo cha Kiislam (Hawza) Imam Swadiq Sheikh Hemed Jalala amesema hatua
zinazochukuliwa na Rais Magufuli zinafanana kwa mbali na Utawala wa Imam Ali (a.s)
ambaye mara nyingi alikuwa anachukizwa na watu kutowajibika katika majukumu yao
na waliokuwa tayari kuwatumikia watu badala ya matumbo yao.
Sheikh Jalala ambaye pia ni Kiongozi mkuu wa Waislamu dhehebu la shia Ithnasheria amesema hayo leo ,Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam, wakati akiongea na Waandishi wa Habari wakati wa kumbukumbu ya kuzaliwa Imam Ali (a.s) na kusema kuwa kama linakuja suala la kufafanisha uongozi basi kwa mbali utawala wa Magufuli unaonekana kufuata nyayo za Utawala wa Imam Ali (a.s).
“Utawala wa Imam Ali (a.s) ni utawala uliogubikwa na Utawala bora ambao ambao ulikuwa unapinga watu au mtu kujilimbikizia pesa, kufanya ufisadi, kutomtanguliza mungu kwa kila jambo, kufuja mali za umma na kuhakikisha watu wote wanakuwa na hali sawa” amesema sheikh Jalala.
"Imam Ali alizaliwa tarehe 13 Rajab mwaka wa 30 wa 'amul-fil' katika Alkaaba takatifu,mjini Makka, Mama yake ni Fatmah bint Asad, Baba yake ni Abu Taalib Ibn Abdul-Muttalib, Kuniya ni Abul-Hassan na Abu -Turab, yeye ndie Khalifa na Imam wa kwanza baada ya kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w)"
Amesema Ukimsoma Imam Ali utagundua kuwa katika utawala wake hakupenda wananchi wa hali ya chini kunyanyasika, na pia alitilia mkazo wa watu wake kutafuta elimu popote pale na kwa hali yoyote
“Jambo hilo pia limeonyesha kwa vitendo na Rais wa awamu ya Tano Rais Dkt. John Joseph Pombe Magufuli hususani pale alipotangaza kuwa Elimu bure hadi kidato cha nne. Ambapo imepelekea watanzania wa hali ya chini kupeleka watotowao Shuleni” amesema sheikh Jalala
Aidha Shekhe Jalala ametaja baadhi ya mambo muhimu ambayo unaweza kuyapata katika utawala wa Imam Ali (a.s) ni jinsi ambayo Imam Ali (a.s) alikuwa akiongoza umma wa watu huku akimtanguliza Mungu.
“Utawala wa Imam Ali ulitawaliwa na hofu ya Mungu jambo ambalo lilisaidia kupunguza vitendo vya ufisadi, vitendo vya kuminya haki za binadamu na watu wengi kuwa na moyo wa kuwajibika” ameongoza Sheikh Jalala
Hatahivyo Shekh Jalal amemaliza kuongea na Waandishi wa Habari kwa kwa kuwataka watanzania wote wakiwemo viongozi wa dini kuhakikisha wamuombee sana Rais wa Tanzania ili aweza kufanikisha lengo lake la kuifikisha Tanzania katika mafanikio ya kimaendeleo.
“Ndugu zangu nataka nitumie fursa hii kupongeza kazi nzuri inayofanywa na Rais John Magufuli, bila shaka kwa kasi anayoenda nayo taifa litapiga hatua kubwa na kufanya wananchi wa hali ya chini kunufaika na rasilimali zilizopo” amesema sheikh Jalala.
No comments:
Post a Comment