Kiongozi wa Waislamu Shia Ithnasheriya Maulana Sheikh Hemed Jalala (wapili kushoto) akiongoza msafara wa Vijana kuelekea katika eneo la Zoezi la Usafi, katika kata ya Kigogo Mkwajuni Dar es salaam. |
Kiongozi wa Waislamu Shia Ithnasheriya Maulana Sheikh Hemed
Jalala amesema kuwa malengo ya Imam Hussein (a.s) ni kuifanya jamii iwe salama,
na katika hali ya usafi wa Mazingira kwani kufanya hivyo ni kutekeleza Mafunzo
ya Dini.
“Tunaamini ya kwamba Moja ya Malengo ya Imama Hussein (a.s)
Mtoto na Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) kutoka na kuelekea katika ardhi ya
karbala ni kufanya jamii iwe salama ni kufanya jamii iwe safi ni kufanya jamii
iwe katika mazingira mazuri, na sisi tunaamini ya kwamba jambo la Usafi ni
jambo kubwa na ni jambo muhimu, tunaamini ya kwamba Uasfi ni katika Imani Usafi
ni katika dini” Maulana Sheikh Jalala
Kiongozi wa Waislamu Shia Ithnasheriya Maulana Sheikh Hemed Jalala akiongea na Waandishi wa Habari punde tu baada yta kuanza zoezi la Usafi. |
Sheikh Jalala alisema hayo jana katika zoezi la Usafi
ulifanyika katika kata ya Kigogo Jijini Dar es salaam kwa lengo la kukumbuka
Kifo cha Imam Hussein (a.s) Mtoto na Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).
“Kutoka kwetu na Kufanya Usafi ni kwa ajili ya kuhakikisha
yakwamba tumemuunga mkono Imam Hussein (a.s) katika jambo lake la kutengeneza
jamii ,tunaamini yakwamba Usafi ni chachu ya kuleta afya bora, tunaamini
yakwamba usafi ni sababu ya watu kukaa katika mazingira mazuri, watu wanaokaa
katika mazingira mazuri watakaa kwa usalama, wanaweza kuwa na elimu bora”
Aidha Sheikh Jalala amesema miongoni mwa sbabu ya kutoka na
kufanya usafi na kuiunga Mkono Serikali ya Mkoa wa Dar es salaam ambayo
yanaenda sambamba na Mafundisho aliyotoka Imam Hussein (a.s) kuyatetea yarudi
katika Jamii iliyomzunguka.
Serikali yetu na Mkoa wetu wa Dar es salaam kwa kupitia Mkuu
wa Mkoa huwa ikipiga kelele marakwa mara
kuhusiana na jambo la usafi mpaka ikaweka siku maalumu ya usafi, tumetoka pia
kumuunga mkono mkuu wa Mkoa kwamba tupo nay eye katika jambo la usafi katika
siku hii ya kumkumbuka Imam Hussein (a.s) Mjukuu na Mtoto wa Mtume Muhammad
(s.a.w.w)”
Mjumbe wa Serikali ya Mitaa wa Kigogo Mkwajuni Mhe. Ibrahim Gogo akiongea na Vyombo vya Habari punde tu baada ya kushiriki katika zoezi la Usafi. |
Kwaupande wake Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Kigogo Mkwajuni
Mh. Ibrahimu Gogo amefurahishwa na kitendo cha Waislamu Shia Ithnasheriya
kufanya Usafi katika eneo lao kwa kuadhimisha Siku ya Kifo cha Imam Hussein
(a.s).
“Sisi kama Watendaji, sisi kama watu wenye dhamana kusimamia
hii serikali katika mtaa wetu, tumeona tuungane nao, tuwe nao pamoja kwasababu
wanafanya jambo la Kijamii ni jambo kubwa, licha ya kuwa wanaadhimisha Kifo cha
Imam Hussein (a.s) wameona tushirikiane katika kusafika maeneo ya mtaa wetu”
Mhe. Gogo.
No comments:
Post a Comment