Thursday, September 12, 2019

“Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uwe na Amani” Sheikh Jalala

Kiongozi wa Waislamu Shia Ithnasheriya Maulana Sheikh Hemed Jalala (wanne kulia) akiongoza Matembezi ya Amani ya Kukumbuka Kifo cha Imam Hussein (a.s) Mtoto na Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ,Kushoto kwake ni Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Mhe. Mousa Farhang.

 Kiongozi wa Waislamu Shia Ithnasheriya Maulana Sheikh Hemed Jalala amewataka Viongozi wa Dini kuweza kumuomba Mungu ili Uchaguzi Ujao wa Serikali za Mitaa uweze kufanyika kwa Salama na Amani bila ya kuleta Vurugu zozote nchini.

Sheikh Jalala ametoa wito huo katika Matembezi ya Amani ya Kumbukumbu ya kuadhimisha Kifo cha Imam Hussein (a.s) Mtoto na Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), yaliyoanzia Ilala Boma na kuhitimishia katika Viwanja vya Pipo Kigogo Post Dar es salaam.

“Wito wetu kwa siku hii ya leo tunaelekea kwenye chaguzi za Serikali za Mitaa, sisi kama Viongozi wa Dini Masheikh, Maustadhi, Maimamu na Maskofu na Wachungaji ni muhimu kwa kweli kumlilia Mungu na kumuomba Mungu Uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa uweze kupita Salama na uweze kupita Vizuri na uweze kupita pasina matatizo yoyote kwasababu ni Uchaguzi Muhimu”

Katibu wa Uchumi wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania (T.I.C) Taifa Mhe. Mohammed Zahoro akiongea na Waandishi wa Habari.
Kwa Upande wake Katibu wa Uchumi wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania (T.I.C) Taifa Mhe. Mohammed Zahoro amewataka Watanzania kuhuisha Mafundisho ya Imam Hussein (a.s) aliyokubali kufa kwa ajili yake.

“Dhulma imejaa, hasadi imejaa hakuna upendo baina ya Waislamu na Waislamu, hakuna upendo Ubinadam na Ubinadamu, hakuna upendo Waislam na Wasiokuwa Waislamu, hakuna upendo baina ya Udugu na udugu, hakuna upendo baina ya Watanzania na Watanzania, tumetoka ili kuyatengemeza hayo ili kurudisha Upendo baina ya watu wote”


No comments: