Watu wasiopungua saba wamepoteza maisha na wengine
wengi kujeruhiwa katika mji mkuu wa Nigeria Abuja kufuatia msongamano wa
maelfu ya watu.
Msongamano huo ulijiri Jumamosi wakati watu
walipokusanyika kuajiriwa katika idara ya uhamiaji. Zoezi hilo lilikuwa
likifanyika katika uwanja wa kitaifa wa michezo Abuja.
Walioshuhudia
wanasema mkanyagano ulijiri pale watu walipojaribu kufika katikati ya
uwanja ambapo kulikuwa na mlango moja tu uliokuwa wazi katika uwanja huo
wenye uwezo wa kubeba watu 60,000.
Bado haijabainika idadi ya watu
waliokuwa ndani ya uwanja wakati wa msongamano huo. Idara ya uhamiaji
Nigeria ilikuwa inaendesha zoezi hilo katika maeneo kadhaa nchini humo.
Ukosefu wa ajira ni changamoto kubwa katika nchi hiyo
tajiri kwa mafuta ya petroli magharibi mwa Afrika ambapo imearifiwa
kuwa asilimia 37.5 ya vijana walio chini ya umri wa
miaka 25 hawana
kazi.irib
No comments:
Post a Comment