Zaidi ya waendesha pikipiki na bajaji 400 wameandamana kuelekea Makao
Makuu ya Chadema, yaliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam kupinga
kitendo cha kukatazwa kuingiza vyombo vyao vya moto katikati ya Jiji.
Vijana hao wakiwa na vyombo vyao vya usafiri pamoja na mabango
yenye ujumbe tofauti walifika kwenye ofisi hizo jana asubuhi wakitokea
maeneo tofauti jijini.
Baadhi ya mabango yao yalisomeka hivi ‘ubakaji, wizi utaongezeka.
Baada ya kuwasili kwenye ofisi hizo, madereva hao walianza kuimba
‘tunamtaka Rais wetu, tunamtaka Rais wetu, peoples power”, wakiimaanisha
Dk. Wilbroad Slaa.
Wakati nyimbo hizo zikiendelea nje ya ofisi hizo, Dk. Slaa alikuwa
hayupo na alipowasili alipokelewa na kelele ‘Rais wetu, Rais wetu, Rais
wetu’. Dk. Slaa ambaye ni Katibu Mkuu wa Chadema, mara baada ya kushuka
kwenye gari lake aliwatuliza vijana hao na kuwaeleza kuwa baada ya
kupata taarifa zao aliwasiliana na vyombo vya dola.
“Nimewasiliana na ngazi zote za polisi akiwamo Mkuu wa Jeshi la
Polisi nchini, kamanda wa jeshi la polisi mkoa na mkuu wa upelelezi na
kukubaliana nao hakuna mabomu,” alisema na kuongeza:
“Mtu anapokimbilia hapa maana yake yupo katika usalama, Chadema
isiyopenda kumwaga damu tunaweza kupata suluhu bila mabomu,” alisema.
Dk. Slaa alisema amezungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said
Meck Sadiki na kwamba amekubali kukutana nao Jumatatu wiki ijayo
No comments:
Post a Comment