Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya mwalimu Nyerere akifungua madahalo katika ukumbi wa Chuo Kikuu (TEKU). Kulia kwake ni Ally Saleh na kushoto kwake ni Pof. Mwesigwa Balegu na Hance Polepole |
Baadhi ya watu waliojitokeza kusikiliza mdahalo katika ukumbi wa Chuo Kikuu (TEKU) |
Wakati
harakati za mashirika yasiyo ya Serikali zikiendelea kutoa elimu juu ya katiba
inayopendekezwa kabla ya kupigiwa kura na kuwa katiba kamili, Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere bwana Joseph Butiku amewataka wananchi
kuipigia kura ya hapana katiba hiyo inayopendekezwa.
Amenukuliwa kuyasema hayo katika mdahalo uliofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu (TEKU) wakati wakitoa maoni yaliyotolewa katika "Tume ya Jaji Warioba" kwamba katiba hiyo haijazingatia kile kilichomo katika rasimu.
Amenukuliwa kuyasema hayo katika mdahalo uliofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu (TEKU) wakati wakitoa maoni yaliyotolewa katika "Tume ya Jaji Warioba" kwamba katiba hiyo haijazingatia kile kilichomo katika rasimu.
“Isomeni
katiba vizuri na kuipigia kura ya hapana kwani mkifanya hivyo italazimu
kuipitia upya kutokana na kwamba katiba inayopendekezwa imeondolewa maono yenu
mengi ikiwepo mamlaka ya Rais, Mbunge kuwajibishwa na wapiga kura wake,
Mawaziri wasitokane na wabunge na kadhalika... wamefanya hivyo kutaka kutetea
maslahi yao na kuwakandamiza wananchi,” amesema Butiku
Naye
mtoa mada, Hance Polepole amesema katiba ni mkataba kati ya wananchi na
viongozi wanao waongoza na hivyo wanatakiwa kuwa makini katika kutengeza
mkataba ili wasije kulaumiwa na vizazi vijavyo kwa kushindwa kutengeneza katiba
yenye kulinda maslahi yao na kuwafanya wengine watumwa katika nchi yao, kwani
kila mtu ana haki ya kufaidi kwa usawa.
Chanzo
No comments:
Post a Comment