Mjumbe wa baraza la maulamaa wa Saudi Arabia na mmoja wa mawahabi mwenye
misimamo ya kufurutu ada ametaka misikiti saba maarufu ya Madina
ibomolewe.
Saleh al-Fawzan, mjumbe wa baraza la maulamaa wakuu wa Saudia
na mjumbe wa kamati ya kudumu ya utoaji fatuwa amedai leo kuwa misikiti
saba ya kihistoria ya mjini Madina ni bid’a na yote inapasa ibomolewe.
Historia ya misikiti hiyo saba inarejea kwenye zama za vita vya Khandaq
na iko kwenye bonde la mlima Sala’a magharibi mwa Msikiti mtukufu wa
Bwana Mtume Muhammad SAW mjini Madina.
Misikiti hiyo saba hivi sasa
imekuwa moja ya maeneo ya ziara kwa Waislamu kutoka nchi mbalimbali
duniani; ambapo mara baada ya kuwasili Madina Waislamu hao huenda kuzuru
misikiti hiyo.chanzo Irib.
No comments:
Post a Comment