Katibu Mkuu wa chama cha Hizbullah cha Lebanon amesema kuwa Marekani
inalitumia kundi la kigaidi la Daesh kuligawa eneo la Mashariki ya Kati.
Sayyid Hassan Nasrullah amesema kuwa Washington na waitifaki wake
wanatumia ugaidi hususan kundi la kigaidi la Daesh kama wenzo wa
kutekeleza mpango wa kuligawa eneo la Mashariki ya Kati, kuanzia Iraq
hadi Syria na hata Saudi Arabia kwa sababu mpango huo unafanyika kwa
maslahi ya Marekani na utawala wa Kizayuni.
Sayyid Hassan Nasrullah
ameyasema hayo jana usiku katika hafla ya kuadhimisha mwaka wa tisa wa
ushindi wa Muqawama wa Lebanon dhidi ya utawala wa Kizayuni katika vita
vya mwezi Julai mwaka 2006.
Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema kuwa upo
udharura wa kupinga na kukabiliana na mpango wa kuligawa eneo hili.
No comments:
Post a Comment