Wakati Umoja wa Katiba
ya wananchi UKAWA ukikumbwa na changamoto ya ugawanaji wa majimbo baada ya
maeneo mengi nchini Tanzania kuibuka migogoro mara baada ya majimbo ya uchaguzi
kugawanywa kwa vyama hivyo,hatimaye mwenyekiti wa chama cha NCCR MAGEUZI ambaye
ni mwenyekiti mwenza wa umoja huo ameibuka na kutoa onyo kali kwa viongozi
ambao wanakuwa wabinafsi wa kutokutaka kuachiana majimbo na kusema kuwa
ubinafsi ni jambo ambalo halitaendekezwa ndani ya umoja huo.
Akizungumza na
wanahabari leo jioni hii Dar es salaam amesema kuwa mara baada ya kukamilika
kwa kazi ya kugawana majimbo kwa vyama vinne vinavyounda umoja huo kumeibuka
sintofahamu ya baadhi ya watu kungangania majimbo ambayo tayari wamepewa watu
wengine jambo ambalo amesema kuwa sio makubaliano ya umoja huo na hawatavumilia
viongozi wa namna hiyo.
Amesema kuwa moja ya
maazimio makubwa ya umoja huo ni kuepuka ubinafsi na kuhakikishya kuwa mambo
wanayoyahubiri kwa wananchi wanayatekeleza kwa vitendo ikiwa ni pamoja na amani
na umoja hivyo hawako tayari kuona chama au mtu yoyote anaanzisha vurugu ndani
ya umoja huo.
Amesema Tayari leo
jioni viongozi wakuu watakutana kuona ni jinsi gani wanaweza kushughulikia
jambo hilo ili ndoto za watanzania za kuhakikisha kuwa wanauondoa mfumo dhalimu
wa CCM uliopo kwa sasa zinatimia na nchi inakuwa na amani na utulivu mkubwa.
No comments:
Post a Comment