Watu watatu wamekufa na wengine
thelathini wamelazwa hospitalini kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa
kipindupindu nchini Tanzania na hasa katika mji wa kibiashara wa Dar es
salaam.
Wataalamu wa afya wamesema kwamba mlipuko huo unapatikana
kwenye maeneo ambayo hayana usafi wa kutosha na vyoo vya kisasa hasa
katika maeneo yenye msongamano wa makazi katika jiji hilo.
Maafisa wa afya tayari wameshachukua hatua ili kuzuia mlipuko huo
usienee zaidi tangu mlipuko mkubwa wa kwanza ulioripotiwa kulikumba jiji
hilo mwaka 2009.
Wodi tengefu kwa wagonjwa wa ugonjwa huo
imeshaandaliwa katika hospitali za wilaya ya Kinondoni eneo ambalo
limeathiriwa vibaya na ugonjwa huo.
Umma wa watanzania wametakiwa kuwa waangalifu baada ya kifo cha
mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka ishirini na saba,mwishoni mwa wiki
iliyopita baada ya kuonesha dalili zinazoshabihiana na magonjwa ya
milipuko.
Dar es salaam ni mmoja kati ya miji yenye idadi kubwa ya watu, mji huo pekee una idadi ya watu zaidi ya milioni tano.
No comments:
Post a Comment