Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo hapa Tehran amesema kuwa kuna
udharura wa kuundwa kamati ya uchunguzi ya kutafuta ukweli ili
kuwatambua wahusika na wanaopaswa kubeba dhima kuhusu maafa ya Mina na
kuvunjiwa heshima miili ya mahujaji walioaga dunia katika maafa hayo
huko Saudi Arabia.
Hujatul Islam wal Muslimin Kadhim Sediqi ameashiria
katika hotuba ya Swala ya Ijumaa ya leo hapa Tehran kuhusu madhara
makubwa ya maafa ya Mina na kusisitiza kuwa madhara na mateso
yaliyosababishwa na maafa hayo yameumiza nyoyo za Waislamu kote
ulimwenguni, na kwamba hayawezi kusahaulika haraka.
Hujatul Islam wal
Muslimin Sediqi amekosoa kadhia iliyo nyuma ya pazia ya utawala wa Aal
Saud kuhusiana na idadi kamili ya mahujaji waliopoteza maisha katika
ibada ya Hija na kueleza kuwa viongozi wa serikali ya Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran wanapasa kufanya juhudi zote na kuwa jadi ili kuweza
kupata ukweli halisi kuhusiana na maafa haya yaliyoathiri ibada ya Hija
ya mwaka huu na kupata ufumbuzi ili kuzuia kukaririwa matukio kama hayo.
Imam wa muda wa Swala ya Ijumaa ya jiji la Tehran amesema kuwepo
udhaifu katika kusimamia marasimu ya Mina ni moja ya sababu kubwa za
kutokea maafa huko Mina na kwamba Saudi Arabia haikufanya jitihada
zozote za kusimamia vyema ibada ya Hija.
Hii ni kwa sababu nchi hiyo hii
leo inafikiria tu kuendesha vita huko Yemen na kuwauwa watu wa nchi
hiyo wasio na hatia. Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran ameongeza
kuwa, ushahidi unaonyesha kuwa baada ya kujiri maafa ya Mina,
polisi wa
Saudia si tu kuwa hawakuchukua hatua yoyote ya maana, bali walishindwa
kufika kwa wakati katika eneo la tukio; polisi badala ya kuwasaidia
mahujaji, waliamiliana vibaya na kwa mabavu na mahujaji waliojeruhiwa na
walioaga dunia mara baada ya kufika katika eneo la tukio. Chanzo Irib
No comments:
Post a Comment