VYA HABARI
Kiongozi wa Chama Ndugu Zitto Zuberi Kabwe
anatoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na
wanachama kwa ujumla kwa kuondokewa na kiongozi mchapakazi, mwadilifu,
mzalendo na aliyekuwa na mapenzi mema na nchi yake.
Amemuelezea Marehemu Mallah kuwa mbali na kuwa
Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Raslimali Taifa pia alikuwa mgombea Ubunge wa
jimbo la Arusha mjini kwa tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo,
Mwenyekiti wa kwanza wa Ngome ya wazee Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya
Chama Taifa.
Kutokana na Msiba huo Kamati ya Uongozi Taifa,
imeagiza kusimama kwa kampeni za ACT-Wazalendo kwa muda wa siku tatu
kuanzia leo tarehe 09 Oktoba hadi Jumapili tarehe 11 Oktoba 2015. Aidha bendera
za chama kwa nchi nzima zitapepea nusu Mlingoti kwa siku tano kuanzia leo
Oktoba 9 – 13, 2015.
Akimuelezea Marehemu Mallah,Zitto,
alisema “Nilimtambua Mzee Estomih Mallah kwa misimamo yake ya kupigania usawa
na amani tokea akiwa katika CHADEMA na hakuogopa kupoteza nafasi ya udiwani
aliyokuwa akiishikilia kwa sababu ya kukataa kuyumbishwa”
Amesema Mallah amefariki akiwa anapigania ukombozi wa watu wa jimbo la
Arusha mjini na kwamba ACT-Wazalendo itamuenzi kwa kukemea yale
maovu yote aliyoanza kukemea na kuendeleza mema yote aliyoyaacha.
“ACT-Wazalendo
itaendelea kumkumbuka daima kwa busara zake na uongozi wake uliotukuka,
alijitoa kulitumikia taifa bila ubaguzi wala upendeleo wowote, hivyo Chama
kitamuenzi kwa kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni,
Taratibu
na Miongozo mbalimbali aliyoshiriki kuiasisi wakati wa uhai wake”
Oktoba 6
mwaka huu, Mzee Mallah alishindwa kupanda jukwaani katika mkutano wa
kampeni za mgombea Urais wa Chama cha ACT-Wazalendo, katika eneo la Ngaramtoni
baada ya kujihisi kizunguzungu na kichwa kumuuma.
Baada ya
hali hiyo alipelekwa katika hospitali ya St. Thomas alipopata mapumziko hadi
jana Oktoba 8 alipohamishiwa hospitali ya KCMC.
Mzee Mallah alifariki dunia wakati madaktari na wauguzi wakiendelea
kumpatia huduma. Taratibu za mazishi zinaendelea nyumbani kwa marehemu.Bwana ametoa, Bwana ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe.
Samson Mwigamba,
KATIBU MKUU.
No comments:
Post a Comment