WAANGALIZI wa muungano wa Ulaya katika
uchaguzi mkuu Tanzania wamesema kuwa tume za uchaguzi za NEC na ZEC
zimejitahidi katika kufanikisha uchaguzi wa amani.
Mkuu wa waangalizi hao Judith Sargentini
amesema kuwa tume hizo mbali na kukabiliwa na changamoto
mbalimbali,lakini wamejitahidi katika kuhakikisha kila raia mwenye haki
ya kupiga kura anapiga kura.
Aidha Judith amesema kuwa kitendo cha
tume hizo kutoa matokeo nusu nusu kumevifanya vyama vya siasa kuanza
kupoteza imani nayo huku wakisema kuwa changamoto hiyo inafaa itatauliwe
haraka ili kuepusha hali ya hatari baadaye.
Amesema kuwa ni vema tume ikaja na matokeo kamili ambayo yatakuwa yamejitosheleza tofauti na jinsi yanavyotangazwa hivi sasa.
Aidha kwa upande mwingine Judith
amevipongeza baadhi ya vyombo vya habari ambavyo vimeonyesha uwajibikaji
stahiki na kuepukana na kupendelea vyama fulani.
Amesema kuwa ni vyema vyombo vingine
ambavyo viliripoti kwa upendeleo vikajifunza kutoka katika vituo ambavyo
havikufanya hivyo kwa kuwa kitendo hicho ni kinyume cha maadili ya
taaluma ya habari.
No comments:
Post a Comment