Tume ya Taifa ya Uchaguzi ( Nec), imesisitiza
kuwa inatangaza matokeo kwa kadiri inavyopokea na siyo kwa kupendelea
upande wowote au kujali aliyeshinda.
Mwenyekiti wa Nec, Jaji mstaafu Damian Lubuva , alitoa ufafanuzi huo jijini Dar es Salaam jana baada ya kutangaza matokeo ya urais katika majimbo 35.
Jaji Lubuva alisema madai yaliyotolewa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuwa wanatangaza matokeo ya maeneo ambayo Chama Cha Mapinduzi kimeshinda ili kuaminisha umma kuwa ni washindi, siyo ya kweli.
"Wakati huu tusingependa kulumbana na chama au vyama vya siasa hata mgombea yeyote, matokeo tunayoyapokea ndiyo tunayatangaza, malalamiko ya kuwa Nec inatangaza kwa mwelekeo wa kupendelea, siyo kweli, tunatangaza bila upendeleo na kujali ameshinda nani," alibainisha.
Alisema siku ya kwanza (juzi), walipokea majimbo matatu na kuyatangaza na kwamba haikuwa rahisi kusubiri majimbo yote ndipo matokeo yatangazwe.

No comments:
Post a Comment