Mamlaka ya mapato Tanzania TRA inaangalia utaratibu wa kutoa bure
mashine za kutolea risiti za EFD’s kwa wafanyabiashara ili kurahisisha
ukusanyaji wa kodi.
Kaimu kamishna mkuu wa TRA Dr.Philiph Mpango amesema hayo wakati
akitoa taarifa kwa vyombo vya habari ambapo amesema mwisho wa watumishi
wa mamlaka hiyo kujaza fomu za mali wanazomiliki ni December 15 huku
akiomba wananchi kusaidia kufichua vitendo vya ufisadi kweneye mamlaka
hiyo.
Kuhusu waliotorosha makontena bila kulipia ushuru amesema
wafanyabiashara 13 tuu ndio wamemaliza kulipa kwa hiari katika muda
uliotolewa na rais na wengine 15 wamelipa sehemu na bado wanadaiwa na
watalazimika kulipa kwa mabavu ambapo kiasi kilichopatikana ni shilingi
bilioni 10.
No comments:
Post a Comment