Waislamu katika maeneo mbalimbali ya dunia leo tarehe 28 Safar
wamekumbuka tukio chungu la kufariki dunia Mbora wa Viumbe na Mtume wa
Mwisho wa Mwenyezi Mungu, Muhammad Mwaminifu, amani ya Mwenyezi Mungu
iwe juu yake na Aali zake. Tarehe 28 Safar.kwa mwaka ni sawa na 11/12/2015.
Mtume Muhammad (s.a.w.w) alifariki dunia tarehe 28 Safar mwaka 11
Hijria akiwa na umri wa miaka 63. Alipewa utume akiwa na umri wa miaka
40 na katika kipindi chote cha miaka 23 aliwalingania wanadamu haki,
upendo, uadilifu na kumwamini Mwenyezi Mungu Mmoja.
Katika siku
za mwisho za uhai wake Mtume (saw) aliwausia mengi Waislamu na kuwataka
washikamane na kufuata vizito viwili ambavyo alisema ni Qur'ani na Watu
wa Nyumba yake tukufu, akisisitiza kwamba hawatapotea iwapo
watashikamana barabara na viwili hivyo.
No comments:
Post a Comment