Wananchi wa Nigeria wamefanya maandamano makubwa ya kulalamikia
kukamatwa na kuendelea kushikiliwa kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya
nchi hiyo, Sheikh Ibrahim Zakzaky.
Televisheni ya Press TV imeripoti kuwa, maandamano hayo yamefanyika
katika mikoa mitano tofauti ya Nigeria na waandamanaji wametaka
kuachiliwa huru mara moja mwanachuoni huyo bila ya masharti yoyote.
Waandamanaji hao wametaka pia kuachiliwa huru mamia ya wafuasi wa Sheikh Zakzaky waliotiwa mbaroni na jeshi la Nigeria.
Mwezi uliopita, jeshi la Nigeria lilifanya mashambulizi ya kikatili
dhidi ya Waislamu katika mji wa Zaria, wakaua na kujeruhiwa watu wengi
na wakamjeruhi vibaya kwa risasi kadhaa Sheikh Zakzaky kabla ya kumtia
mbaroni na kumpeleka kusikojulikana.
Harakati ya Kiislamu ya Nigeria imesema kuwa, makumi ya Waislamu
wanaendelea kushikiliwa na jeshi licha ya hali zao kuwa mbaya kutokana
na majeraha. Aidha imesema, jeshi la Nigeria linawanyima hata matibabu
majeruhi hao. Kwa uchache mmoja wa Waislamu hao ameshafariki dunia
kutokana na majeraha.chanzo irib
No comments:
Post a Comment