Madhehebu
ya kiislam Nchini kote na duniani wametakiwa kujenga umoja wa kudumu,kukaa kwa
pamoja na kujadili maswala yanayowahusu jambo ambalo litasaidia kuleta amani
baina ya dini ya Kiislam na dunia kwa ujumla.
Rai hiyo
imetolewa Jijini Dar es salaam na sheikh Mkuu
wa mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhadi
Mussa Salim wakati wa sherehe ya maalum ya mauled iliyowakutanisha
waislam wa Madhehebu ya SHIA na SUNNI kwa ajili ya kusherekea na kukumbaka kwa
pamoja siku ya kuzaliwa kwa mtume muhammad (s.a.w.w), Masjid Udoe Jijini Dar es salaam.
“Sisi sote ni wana wa Mungu, na tuna muabudu Allah,
kwa hiyo kuna mambo ya msingi yanayotuunganisha na kututenga ndiyo maana unaona
masheikh wa Kisuni wanashirikiana na Washia,” alisema Sheikh Mkuu.
Sheikh Salim amesema kuwa
hakuna haja ya kuendelea kujenga chuki na uhasama baina ya madhehebu hayo bali
jambo sahihi ni kukaa kwa pamoja na kujadili mambo yanayowahusu na yale
yatakayoshindikana kutokana na itikadi za kidini yaachwe ili yasiwe ni chanzo
cha chuki mbalimbali.
“Licha ya tofauti
tulizonazo ni tofauti zitaendelea kuwepo, lakini sisi sote ni Waislam kwa
sababu sote tunaunganishwa Mtume Muhammad (s.a.w.w), Upweke wa Allah (swt),
Malaika, Siku ya Mwisho na Kusimamisha Swala,hivyo hakuna ulazima wa kulumbana
na kutoshirikiana” amesema sheikh Mkuu.
Kwa upande wake Sheikh MSABAHA SHABAN MAPINA (SHIA) amesema kuwa sherehe ya
kukutana kwa madhehebu hayo mawili yenye imani Tofauti tofauti ni jambo la
kuigwa na Tanzania nzima pamoja na dunia kwani ni njia nzuri ya kujenga umoja
wa kidini ambao ilikuwa umeanza kutetereka .
Sherehe hizo za kumbukumbu ya
kuzaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) zimeandaliwa Taasisi ya Kidini ya Kiislam ya
Bilal Muslim Mission of Tanzania na Ilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali kutoka
BAKWATA TAIFA NA MKOA WA DAR ES SALAAM. Muft wa Tanzania Abubakar Zuberi, Sheikh
wa Mkoa wa Dar es salaam Alhad Mussa Salim
No comments:
Post a Comment