Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa,
kujitokeza kwa wingi na kwa mwamko wananchi wa Iran katika chaguzi mbili
zijazo za Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) na ule wa
Baraza la Wanavyuoni Wataalamu la kumchagua na kusimamia kazi za
Kiongozi Muadhamu kutabatilisha njama za maadui.
Ayatullah Ali Khamenei amesema hayo leo wakati huu wa kukaribia
maadhimisho ya tukio la Februari 18, 1978 la wananchi wa Tabriz, mbele
ya maelfu ya wananchi wa matabaka mbalimbali wa mkoa wa Azerbaijan
Mashariki na kusisitiza kuwa, chaguzi mbili za tarehe 26 mwezi huu wa
Februari ni dhihirisho la mwamko wa wananchi wa Iran katika kuulinda
mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu, uhuru na heshima ya taifa lao.
Amesisitiza
kuwa, kushiriki kwa wingi na kwa mwamko wananchi katika chaguzi hizo
kutafelisha tamaa ya maadui wanaotaka wananchi wa Iran wasusie chaguzi
hizo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, adui
anafanya njama za kila aina ili afikie malengo yake kupitia uchaguzi,
hivyo wananchi wa Iran ambao ndio wamiliki hasa wa nchi hii, wanapaswa
kuelewa uhakika wa mambo na kutoruhusu kufanikiwa njama hizo za adui.
Amesema siasa za Marekani na nchi nyingi za Ulaya ziko chini ya
ushawishi na ubeberu wa kanali za Kizayuni na kusisitiza kuwa, hata
hatua zilizochukuliwa na Wamarekani katika kadhia ya nyuklia, navyo
vinapaswa kuangaliwa kwa jicho hilo hilo.
Aidha Ayatulah Khamenei amewashukuru wananchi kwa kujenga hamasa ya
kipekee kwenye maandamano ya kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya
Kiislamu tarehe 11 mwezi huu wa Februari na kuongeza kuwa, jambo hilo
linaonesha namna wananchi wa Iran walivyo macho, wasivyotetereka na
walivyo na azma ya kweli ya kufanikisha malengo yao matukufu.Chanzo irin
No comments:
Post a Comment