Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni ameiomba Ujerumani iinasihi
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ikubali
kubadilishana mateka wa Kipalestina kwa viwiliwili vya wanajeshi wawili
wa utawala wa Kizayuni vilivyoko mikononi mwa Hamas.
Mtandao wa habari wa Palestine Today umemnukuu Benjamin Netanyahu,
Waziri Mkuu wa utawala ghasibu wa Kizayuni akiliambia gaeti moja la
Israel kuwa, viongozi wa Ujerumaini wamekubali kuwa wapatanishi katika
suala zima la kubadilishana na Hamas, mateka wa Kipalestina kwa
viwiliwili vya wanajeshi wawili wa Israel.
Amesema, katika miaka ya huko nyuma pia Ujerumaini iliwahi kuisaidia
Israel katika suala kama hilo, hivyo hivi sasa anaiomba tena iusaidie
utawala wa Kizayuni.
Wanamapambano wa Palestina waliwateka nyara wanajeshi hao vamizi wa
Israel wakati walipouvamia Ukanda wa Ghaza katika mashambulizi ya siku
50 yaliyoanzishwa na Israel dhidi ya ukanda huo uliozingirwa kila
mahali.Chanzo irib
No comments:
Post a Comment