Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema njia pekee ya kupunguza
kuenea athari mbaya za ugaidi na madudu yake ni kupitia kuundwa jela ya
aina yake itakayotumiwa kuwafungia watu wenye misimamo mikali.
Rais Kenyatta amesema kuchanganyika wafungwa wa kawaida na wale wenye
misimamo mikali na magaidi kumechangia tatizo hilo kuenea na watu wengi
kujiunga na makundi ya aina hiyo.
"Tutaunda jela maalumu kwa ajili ya watu wenye misimamo mikali.
Hatutokubali fikra za ugaidi na misimamo mikali kuenezwa kupitia jela za
nchi hii" amesema kiongozi huyo.
Ingawa hakutaja kundi lolote moja kwa moja, wachambuzi wanasema kundi
la kigaidi la al Shabaab ndilo lililolengwa kwenye kauli hiyo ya Rais
wa Kenya.
Kundi hilo limekuwa likifanya mashambulizi ya kushtukiza dhidi ya
raia na maafisa wa usalama wa Kenya ndani na nje ya nchi hiyo.
Shambulizi la hivi karibuni la kundi hilo dhidi ya Kenya ni lile
lililotokea katika kambi ya el-Adde ambako wanajeshi zaidi ya 50 kutoka
Kenya waliuawa.Chanzo irib
No comments:
Post a Comment