Jeshi la Nigeria limesema kuwa, limefanikiwa kuharibu kambi za
wapiganaji wa kundi la kigaidi la Boko Haram katika vijiji vya Doro na
Kuda vya kaskazini mashariki mwa jimbo la Borno.
Msemaji wa jeshi la Nigeria, Kanali Sani Usman, amewaambia
waandishi wa habari kwamba wanamgambo wanne wa Boko Haram wameuawa huku
wengine wawili wakikamatwa wakati wa operesheni katika misitu ya eneo la
Alagarno na Sambisa.
Wanajeshi watatu na raia wanne wamejeruhiwa katika
mapigano kati ya wanamgambo hao na maafisa wa usalama.
Jeshi la Nigeria limesema operesheni kama hizo zitaendelea katika
maeneo mengine ya nchi hiyo hadi pale kundi hilo la kitakfiri
litakapozidiwa nguvu na kutokomezwa.
Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria amesisitizia umuhimu wa ushirikiano
wa mataifa ya Afrika Magharibi na Kati ili kufanikiksha vita dhidi ya
ugaidi.
Kundi la Boko Haram limepoteza eneo kubwa lililokuwa likilidhibiti,
lakini bado linafanya hujuma za kushitukiza dhidi ya maeneo ya raia na
kusababisha maafa na hasara kubwa.Chanzo irib
No comments:
Post a Comment