Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii
, Jinsia , Wazee na Watoto Ummy Mwalimu leo ametembelea Hospitali ya
Taifa Muhimbili-MNH- kwa lengo la kukagua jengo la watoto pamoja na
jengo la wazazi namba mbili ( Maternity Block Two) ili kuona utendaji
kazi na utekelezaji wa maagizo ya Rais John Magufuli .
Mwishoni mwa wiki iliyopita,
Rais Magufuli aliagiza watumishi wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii
, Jinsia , wazee na Watoto kitengo cha afya ya mama na mtoto kuhama
katika jengo hilo ili kupisha Hospitali ya Taifa Muhimbili kulitumia
kama wodi ya wazazi .
Waziri Ummy ambaye ameambatana
na Naibu Waziri Dokta Hamis Kigwangala ameelezea kuridhishwa na
ukarabati unaoendelea katika majengo hayo .
“Jengo la watoto tatizo kubwa
lilikuwa ni miundombinu ya maji lakini naona ukarabati unaendelea
vizuri na nina imani kuwa ukarabati utakamilika kwa wakati” amesema
Waziri .
Akizungumzia kuhusu jengo la
wazazi namba mbili , Waziri huyo wa afya amesema kuwepo kwa jengo hilo
ni faraja kwa kina mama na kusisitiza kwamba hakuna mama mjamzito
atakayelala chini .
Mpaka sasa kina mama 53 tayari wamehamia katika jengo hilo na wanapatiwa huduma zote.
No comments:
Post a Comment