Ayatullah Naser Makarem Shirazi mmoja wa Marajii Taqlidi wa
nchini Iran amesema kuwa, viongozi wa Kiarabu katu hawawezi kuficha
mafanikio ya kujivunia ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Hizbullah
ya Lebanon.
Kiongozi huyo wa kidini mwenye makao yake mjini Qum hapa Iran
amebainisha kwamba, hatua ya viongozi wa Kiarabu ya kupasisha maazimio
ya aibu dhidi ya Hizbullah katu haiwezi kuficha mafanikio ya kujivunia
ya harakati hiyo ya mapambano, kwani Hizbullah itaendelea kubakia kuwa
ni shujaa na bingwa.
Ayatullah Makarim Shirazi ameongeza kwamba, historia ya Waarabu
imeshuhudia mara chache sana ushujaa na ujasiri kama wa Hizbullah ya
Lebanon kwani harakati hiyo imeweza kuushinda utawala ghasibu wa Israel
uliokuwa haushindwi.
Ikumbukwe kuwa, Jumatano iliyopita Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya
Uajemi liliiweka harakati ya Hizbullah ya Lebanon katika orodha ya
makundi ya kigaidi na kutangaza kuwa, limechukua hatua kadhaa katika
uwanja huo. Hatua ya baraza hilo linaloundwa na nchi za Saudi Arabia,
Qatar, Kuwait, Oman, Umoja wa Falme za Kiarabu na Bahrain imekabiliwa na
upinzani mkubwa ndani na nje ya Lebanon.
Asasi na harakati mbalimbali
za kieneo na kimataifa zimelaani vikali hatua hiyo ya Baraza la
Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi.Chanzo irib
No comments:
Post a Comment