Asksari wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamewaua shahidi
Wapalestina 200 tangu ilipoanza Intifadha ya Quds mwezi Oktoba mwaka
jana hadi hivi sasa.
Jumuiya ya kitaifa ya familia za mashahidi wa Palestina leo imetoa
ripoti inayoeleza kwamba tangu ilipoanza Intifadha ya Quds mwanzoni mwa
mwezi Oktoba mwaka jana hadi sasa, Wapalestina 200 wameuliwa shahidi
katika maeneo tofauti ya Ufukwe wa Magharibi, Ukanda wa Gaza na vilevile
katika mji wa Baitul Muqaddas.
51 miongoni mwa mashahidi hao ni watoto wadogo na 20 ni wanawake.Kwa mujibu wa ripoti hiyo, katika muda wa saa 48 zilizopita
Wapalestina saba wameuawa shahidi, watano huko Baitul Muqaddas na wawili
katika eneo la Ufukwe wa Magharibi.
Tangu mwanzoni mwa mwezi Oktoba mwaka uliopita wa 2015 hadi sasa
maeneo mbalimbali ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu yamekuwa
yakishuhudia wimbi la malalamiko ya upinzani dhidi ya siasa za
kichokozi za utawala wa Kizayuni na njama za utawala huo za kupotosha
utambulisho wa Baitul Muqaddas pamoja na mpango wake wa kuugawa kiwakati
na kimahali msikiti mtukufu wa Al-Aqsa. Wimbi hilo la malalamiko
limekuwa maarufu kwa jina la Intifadha ya Quds.chanzo irib
No comments:
Post a Comment