Monday, April 4, 2016

Watoto wenye Usonji wanamahitaji kama watoto wa Kawaida Tusiwatenge

Serikali ya Tanzania imesisitiza kuwa itaendelea kutoa elimu bora na Bure kwa watoto wote wa kitanzania bila kubagua rangi,kabila wala dini huku mkazo mkubwa sasa ukielekezwa pia kwa watoto wenye ulemavu na mahitaji maalum lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa watoto wote wa Tanzania wanapata elimu sawa.

"Aidha niwatake  wazazi, walezi na jamii bila ya kujali tofauti za kimaumbile kuhakikisha watoto wote wanapata fursa ya elimu, pia jamii inapaswa kuwachukulia watu wenye mahitaji maalumu kama ni sehemu muhimu ya jamii na wanasshirikishwa kikamilifu katika nyanja zote za Maendeleo" amesema Dr. Manyanya

Kauli hiyo hizo zimetolewa na Naibu waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Dr. Stella Manyanya akishiriki matembezi ya maadhimisho ya siku ya watu wenye usonji Duniani ambayo imeadhimishwa leo Jijini Dar es salaamMaandamano hayo yameratibiwa na shule ya Al Muntazar na kushirikisha matabibu, waalimu wanafunzi, Changamoto kubwa ikiwa ni uelewa mdogo miongoni mwa jamii kuhusu ulemavu huo.

Huku wengine wakiuchanganya ulemevu huo na mtindio wa ubongo, wengine wanauhusisha na imani za kishirikina,jambo ambalo limesababisha ugumu katika matunzo ya watoto wenye Usonji" anasema Dr Stella Rwezaura, rais wa chama cha watu wenye Usonji Tanzania.

Usonji ni upungufu wa kibaiologia anaopata mtoto anapokuwa tumboni kwa mama yake na dalili zake huonekana kuanzia umri wa miaka mitatu na kuendelea ambapo.

Maadhimisho ya watu wenye usonji huazimishwa kila tarehe 2, ya mwezi april ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ilikuwa “TUWAPENDE NA TUWALINDE.Picha zaidi Bofya chini.
 
Hatahivyo Dr. Manyanya amesema kuwa Serikali kwa ikishirikiana na sekta binafsi na wadau wa elimu imekuwa ikipanua fursa za upatikanaji wa elimu kwa watoto wenye mahitaji maalumu kwa kuandaa walimu, kuboresha miundombinu na kutoa kipaumbele kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika elimu.

"Napenda kuipongeza Taasisi yenu ya Almuntazir kwani imekuwa mstari wa mbele katika kuwahudumia watoto wenye usonji na wenye mahitaji mengine maalumu kwa kuwapatia elimu na huduma nyingine za Kijamii" amesema Dr. Manyanya

Naibu waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Stella Manyanya akishiriki matembezi ya maadhimisho ya siku ya watu wenye usonji Duniani ambayo imeadhimishwa leo Jijini Dar es salaam



Naibu waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Stella Manyanya akishiriki matembezi ya maadhimisho ya siku ya watu wenye usonji Duniani ambayo imeadhimishwa leo Jijini Dar es salaam

No comments: