Thursday, July 7, 2016

"Ni aibu kwa Watanzania Kuzungumzia Ushoga"Sheikh Jalala

Masheikh Mbalimbali kutoka katika Jumuiya ya Shia Ithnasheriya Tanzania na Hawzat Imam Swadiq wakiswali swala ya pamoja ya Eid Fitri jana katika uwanja wa Pipo Kigogo Post Dar es salaam, chini ya Uongozi wa Kiongozi Mkuu wa Waislam dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala





Viongozi mbalimbali wa Jumuiya ya Shia Ithnasheriya Tanzania wakijumuika pamoja na Waumini wenzao katika swala ya Eid Fitri jana Dar es salaam,(kulia) ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Taifa ni Mzee Brigedia Simba

Kiongozi Mkuu wa Waislam dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akiswalisha waumini mbalimbali wa kike na wakiume swala ya Eid Fitri, jana katika uwanja wa Pipo Kigogo Post, Dar es salaam
 "Sisi Watanzania na sisi Waislam ilikuwa sio jambo la kawaida midomo yetu kutamka neno Ushoga ni jambo la aibu halitamkwi jambo hili kwa kiswahili,leo hii neno Ushoga tunaweza kulitamka kwenye mimbari zetu, lakini mbaya zaidi ya hivyo leo hii tunapata redio za Tanzania zinamuhoji mtu anaebeba Ushoga,

 hatari kubwa inayokuja kwa Watanzania, ni jambo la kutisha,ushoga hauna nafasi kwa Waafrika ni jambo la aibu ni jambo la kutisha lisifanwe kuwa jambo la kawaida na kuzungumzwa ndani ya Vyombo vya Habari"alisema Sheikh Jalala.

Sheikh Jalala alisema hayo jana katika khutba ya swala ya Eid Fitri, iliyoswaliwa katika kiwanja cha Pipo Dar es salaam,na kuhudhuriwa na mamia ya Waumini wa kike na wa kiume.







Ushoga, ni uhusiano wa mapenzi wa watu wa jinsia moja, ni marufuku nchini, kwa mujibu wa Sheria ya Adhabu.

Kwa mujibu wa Sura ya 16, sehemu ya 154, mtu anayejihusisha na ngono na mtu mwingine kinyume na maumbile au anayemruhusu mtu mwingine kufanya naye ngono kinyume na maumbile, atakuwa amefanya kosa la jinai na kustahili kifungo cha miaka 14 jela.

No comments: