Thursday, July 7, 2016

"Tusiwaache Mayatima wakirandaranda Mitaani"Sheikh Abdi


Hawa ni baadhi ya watoto Yatima waliohudhuria  futari ya pamoja na Masjid Ghadir,Kigogo Post Dar es salaam, iliyoandaliwa na Uongozi wa Chuo cha Kiislam (Hawzat) Imam Swadiq Chini ya Kiongozi Mkuu wa Waislam dhehebu la ShiaIthnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala.

Naibu wa Chuo cha Kiislam (Hawzat) Imam Swadiq Sheikh Muhammad Abdi akielezea jambo katika futari hiyo ya Mayatima Dar es salaam.
 Katika hafla hiyo kwaniaba ya Sheikh Jalala, Naibu wa Chuo cha Kiislam (Hawzat) Imam Swadiq Sheikh Muhammad Abdi Mbwana, amesema kuwa kitendo mtoto kupatwa na uyatima halafu jamii inamuacha hadi anakuwa Ombaomba sio uungwana na ni jambo la aibu ambalo halikubaliki.
  
"Jamii na serikali kwa ujumla kuwangalia watu hao kwa jicho la karibu zaidi kwa kile alichodai hata wao hawakuomba wala kutaka kuondokewa na wazazi au mzazi duniani, ambapo ameongeza kuwa kufanya Ihsani kwa yatima ni moja ya sehemu ya dini" alisema Sheikh Abdi






Katika muendelezo wa kufuturisha makundi maalumu katika jamii, baada ya kufanya hivo kwa kamati ya Amani Jijini Dar es salaam, Wajane, watu wenye ulemavu wa Ngozi,  jioni ya leo Kiongozi mkuu wa waislamu wa dhehebu la Shia Ithna-sheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala amewaongoza waumini wa Msikiti wa Kigogo Post wa Ghadir Jijini Dar es salaam, katika futari ya Pamoja na watoto yatima.

No comments: