Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza amesema
kuwa, raia 130 wa nchi hiyo wanachama katika kundi la kigaidi la Daesh
wameuawa nchini Syria.
Boris Johnson ameliambia Bunge la Uingereza kwamba, karibu
Waingereza 850 wamekwenda Syria na kujiunga na kundi la kigaidi la Daesh
tangu mwaka 2011 na kwamba karibu nusu yao wamerejea nchini.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza amesema kuwa, idadi ya raia wa
nchi hiyo wanaojiunga na kundi la Daesh na makundi mengine ya kigaidi
huko Syria imepungua na kuongeza kuwa, propaganda za kundi la kigaidi la
Daesh zimepungua kwa asilimia 70 kuanzia mwaka jana wa 2015.
Boris Johnson amesisitiza kuwa, kundi la kigaidi la Daesh
linadhoofika siku baada ya siku na kwamba kundi hilo litaangamizwa
kikamilifu baada ya kukombolewa mjini wa Raqqa nchini Syria ambayo ndio
ngome kuu ya magaidi hao.
Serikali ya Syria na washirika wake wanapambana na wapiganaji wa
makundi ya kigaidi hususan Daesh na Jabhatu Nusra ambayo yaliingia
nchini humo kwa msaada wa nchi kama Marekani, Saudi Arabia, Uturuki na
washirika wao
No comments:
Post a Comment