Mkuu wa Siasa za Nje za Umoja wa Ulaya amesema kuwa ni haki ya watu wa nchi za bara hilo kuisusia Israel.
Federica Mogherini ambaye alikuwa akijibu maswali ya mwakilishi
wa Ireland katika Bunge la Ulaya kuhusu harakati ya kuususia utawala wa
Kizayuni wa Israel (BDS) amesema kuwa, haki ya uhuru wa kujieleza watu
wanaotaka kushiriki katika kuisuia Israel inapaswa kuheshimiwa.
Mkuu wa
Siasa za Nje za Umoja wa Ulaya amesisitiza kuwa, Ulaya inaunga mkono na
kutetea uhuru wa kujieleza wa jumuiya mbalimbali ikiwemo ile ya kuisuia
Israel.
Federica Mogherini ameyasema hayo akijibu maswali ya mwakilishi wa
Ireland katika Bunge la Ulaya, Martina Anderson ambae ni miongoni mwa
watetezi wa haki za Wapalestina.
Anderson alimtaka Mkuu wa Siasa za Nje
za Umoja wa Ulaya, Bi Mogherini aweke wazi misimamo yake kuhusu harakati
ya kuisusia Israel barani Ulaya maarufu kwa kifupi kwa jina la BDS.
Msimamo wa wazi wa Federica Mogherini wa kutetea haki ya watu wa
Ulaya kuisusia Israel umekaribishwa kwa mikono miwili na harakati
mbalimbali za kupigania ukombozi wa Palestina inayokaliwa kwa mabavu na
Israel.
No comments:
Post a Comment