Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina
akizungumza na Viongozi wa Bandari ya Dar es salaam mara baada ya
kuwasili Bandarini hapo kwaajiri ya kufanya ziara.
Na: Twalha Ndiholeye – DAR ES SALAAM
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mzingira Mhe. Luhaga Mpina
amefanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Dar es salaam ili
kujionea utaratibu wa Bandari hiyo wa kuondosha taka zitokanazo na
shughuli zake.
Ziara
ya Naibu Waziri Mpina imetokana na Malalamiko ya wananchi yaliyodai
kuwa uchafuzi mwingi umekuwa ukifanyika katika Bahari na sehemu kubwa ya
fukwe ya bandari imekuwa ikijaa taka za aina mbali mbali.
Kutokana
na malalamiko hayo ya wakazi wa jiji la Dar es Saalam, Naibu Waziri
kabla ya kukagua maeneo ya kutoa na kukusanya taka za aina mbali mbali
katika bandari hiyo zikiwemo taka za mafuta ghafi, alipokea taarifa
kutoka kwa uongozi wa Bandari ambapo ameshangazwa na kile kilicholezwa
na Afisa Mazingira wa bandari Bwana Thobias Sonda kuwa Bandani hiyo
kubwa katika kanda ya Afrika Mashariki haina sehemu ya kupokea taka
yaani waste reception facility na haina takwimu za taka zinazoingia na kutoka Bandarini Hapo.
Akishindwa
kujibu Baadhi ya Maswali yaliyoulizwa na Naibu Waziri Mpina Afisa
mazingira huyo alieleza kuwa, Bandari hiyo inazalisha aina mbili kubwa
za taka ikiwa ni taka za aina mbali mbali na taka za maji taka, alisema
kuwa taka hizo zinaondoshwa na wakala ambao wanasajiliwa na Sumatra lakini
haikueleweka wazi kuwa, taka hizo zinatupwa wapi na aliongeza kwa
kusema kuwa, taka nyingi na hali ya uchafu inayoonekana pembezoni mwa
Bandari ya Dar es Salaam inatokana na shughuli za kibinadamu kiwandani
hapo, na kusema kuwa, kuna utaratibu wa kufanya usafi na kuziondosha na
kukanusha kuwepo kwa taarifa za boat na meli zinazofanya safari za kuanzia bandarini hapo kuchafua mazingira ya bandari na Bahari.
Afisa
Mazingira huyo, liongeza kwa kusema kuwa taka za maji taka pamoja na
kukosekana kwa takwimu za uondoshwani na umwagaji, zimekuwa
zikikuswanywa a magari yao maalumu na kumwagwa katika mabwawa yao
yaliyopo Kurasini jijini Dar es Salaam.
Kwa
kushangwazwa na hali hiyo, Mpina kupitia Baraza la taifa la Hifadhi na
Usimamizi wa Mazingira NEMC ameutaka uongozi wa Bandari hiyo kujenga
mfumo mzuri wa kuhifadhi taka kwa muda wa miezi sita na kuripoti kwa
Baraza za Mazingira kwa miezi mitatu Mfulizo kuonyesha namna ambavyo
uondoshaji wa taka hizo unafanyika, Pamoja na kuwasilisha ripoti kwa
Baraza ya Namna ambavyo mawakala hao walipatikana.
Aidha
Naibu waziri Mpina ameliagiza baraza kumpelekea ripoti ndani ya siku
saba, inayoonyesha kama hao mawakala wa kukusanya taka bandarini wapo
kisheria.
Kwa
Upande wake Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Bandari Nchini Bw. Nelson Mlele
amesema kuwa amepokea maagizo ya Mhe kupitia NEMC kwani yanawakumbusha
utekelezaji wa majukumu yao na kwa upande wa Bandari ni changamoto
itakayofanyiwa kazi haraka.;
No comments:
Post a Comment