Friday, June 9, 2017

"Tutaendelea Kuiombea Tanzania yetu Amani "Sheikh Alhad

Sheikh Alha,  Mussa Mwenyeliti wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Dar es salaam, ambae pia ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam akiongwa katika Hafla ya Futari ya Pmoja na Kamati ya Amani na Viongozi wa Dini, Masjd Ghadir, Kigogo Post Dar e salaam.
KAMATI ya amani ya Mkoa wa Dar es Salaam, imesema itaendelea kuombea amani ya nchi na kwamba haitamvumilia mtu atakayehamamsisha watanzania wafanye fujo na kuvunja amani iliyopo.
 
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Shekhe wa mkoa huo, Alhad Mussa Salum alisema hayo wakati wa futari ya pamoja ya viongozi wa dini iliyoandaliwa na Chuo cha Kiislamu cha Imam Swadiq kilichopo Kigogo Post.

Alisema mtu anayehamasisha watu kuvunja amani kwa kijana kwa kisingizio cha dini, wanamtilia shaka imani yake kwani sio misingi ya dini.


Alifafanua kuwa dini zote zinaelezea umuhimu wa kuenzi amani iliyopo kwani hata salamu zao kati ya wakristo na waislamu zinatangaza amani kwa kila mtu.

"Waislamu wamekuwa wakizungumzia mahusiano mema kati yao na madhehebu mengine lakini pia mahusiano haya yanahitajika miongoni mwa madhehebu yaliyomo ndani ya dini yetu kama vile Sunni na Shia," alisema Shekhe Salum.

Aliongeza kuwa wapo watu wanaojihusisha na mambo maovu kwa kisingizio cha dini, ukweli ni kwamba hakuna dini inayomtuma mtu kufanya mauaji bali wanahamasisha kuenzi amani iliyopo na kupinga vitendo hivyo.
Image may contain: 2 people, people standing, beard, hat and text
Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akiongea katika Hafla ya Futari ya Pmoja na Kamati ya Amani, Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam.

Naye, Kiongozi wa Shia Inthasheriya, Shekhe Hemed Jalala alisema malengo ya kuwakutanisha kamati ya amani ni kuhakikisha mkoa wa Dar es Salaam na nchi kwa ujumla inakuwa na amani.

"Tunataka wakristo na waislamu kuendelea kuishi kwa amani, upendo na maelewano. Pia kwa ushirikiano wetu tutasaidia mkoa huu kuwa na amani na kuombea Taifa letu lizidi kuwa na umoja," alisema Shekhe Jalala.

Pia alisisitiza kuwa ni lazima kuombea amani isipotee kwa kuwa ndio sababu ya kuwa na uhuru wa kuabudu, kufanya kazi na mshikamano.

No comments: