Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Maulana Sheikh Hemed Jalala akiongea katika Khutba ya Swala ya Ijumaa, leo Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam. |
Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Maulana Sheikh Hemed Jalala
amewataka Waislamu wa Tanzania kuienzi amani, Umoja kwa kuacha tofauti ya
Mitazamo yao pamoja na kujitenga na makundi yenye lengo la kuondoa Umoja na
Mshikamano baina ya Waislamu na Watanzania.
Maulana Sheikh Jalala amesema hayo leo katika Khutba ya Swala ya
Ijumaa ya wiki iliyopita, iliyoswaliwa Masjid Ghadir, Kigogo Post, Jijini Dar
es salaam, huku akizungumzia Je, Uwahabi na Usuni ni Kitu Kimoja?.
“Katika zama hizi ni zama ambazo Waislamu wanahitajia kuwa
kitu kimoja,kama kuna kipindi Waislamu wanatakikana waache tofauti zao,na
mitizamo zao ni zama tulizokuwa nazo, ni zama ambayo Umoja, kuwa kitu kimoja,
kuzungumza pamoja, kukaa meza moja, ni zama muhimu mno” Alisema Maulana Sheikh Jalala.
Aidha Maulana Sheikh Jalala anawakumbusha Waislamu wa Tazania
kuwa asili ya Watanzania hata kabla ya Uhuru na baada ya Uhuru wameleleka
katika Umoja, kupendana, kushirikiana, kuelewana, kusaidiana bali hawakuleleka
katika kubaguana na kukufurishana.
“Watanzania wameleleka
kwenye Umoja, kupendana, kuelewana, kushirikiana, watanzania hawajaleleka
kwenye kubaguana na kuchukiana Waislamu wa Tanzania Ahlul Sunna, Shia
Ithnasheriya na Ibaadhi katika nchi hii walikuwa kitu kimoja hata kabla ya
Uhuru wa nchi hii,na wala hawakujua kubaguana, wala kukufurishana” alisisitiza
Maulana Sheikh Jalala
Hatahivyo Maulana Sheikh Jalala amewatahadharisha Waislamu na
Watanzania kujitenga na makundi yote likiwemo kundi la Kiwahabi yenye malengo
mabaya ya kuichafua Tanzania inayosifika nchi ya Amani na Maelewano.
“Malengo la
kundi hilo la Kiwahabi ni kutaka kuwagawa na kuwataka kuwafanya kuwa ni makundi
tofauti ambayo mwisho wa yote ni kugombana na kuifanya Tanzania sio mahala pa
amani, maelewano na mshikamano”aliongeza Maulana Sheikh Jalala
No comments:
Post a Comment