Vyakula vilivyotolewa na Rais Jakaya Kikwete vikiwa eneo la tukio vikisubiri kuchukuliwa. |
Mwakilishi wa Kituo cha Wazee na Wasiojiweza cha Nunge kilichopo Kigamboni, David Mpangala akiwa na mbuzi waliotolewa kwa ajili ya kituo hicho. |
RAIS
Jakaya Kikwete ametoa zawadi ya vyakula na kitoweo kwa makundi
mbalimbali kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Idd El Haji ambayo
inaadhimishwa duniani kote leo.
Zawadi
hiyo imekabidhiwa kwa makundi hayo kwa niaba yake na Kamshna Msaidizi
Kitengo cha Walemavu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Beatrice
Fungamo Dar es Salaam leo asubuhi.
Akizungumza
na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi zawadi hiyo, Fungamo alisema
Rais ametoa zawadi hiyo kwa ajili ya Sikukuu ya Idd El Haji kama
anavyofanya siku zote wakati wa sikukuu mbalimbali.
Fungamo
alitaja vituo vilivyopata zawadi hiyo kuwa ni Mahabusu ya Watoto ya
Upanga iliyopo Manispaa ya Ilala, Makazi ya Wazee wasiojiweza ya Nunge,
Kigamboni, Chuo cha Watu wenye Ulemavu cha Yombo Temeke na Kituo cha
Kulelea Watoto Mayatima (Chakuwama) cha Sinza.
Alitaja
vituo vingine kuwa ni Kituo cha Makao ya Watoto Yatima cha Mburahati,
Ilala, Kituo cha Makao ya Watoto-Kurasini, Kituo cha Full Gospel, Temeke
na Kituo cha Watoto Alsaad Children House Kurasini.
Alivitaja
vituo vingine kuwa ni cha Vosa Mission cha Kongowe, Temeke na Kituo cha
Kijiji cha Furaha kilichopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Fungamo
alitaja vituo vilivyopata zawadi hiyo ya Idd El Haji kwa upande wa
Zanzibar kuwa ni Kituo cha Mabaoni kilichopo Pemba na Makazi ya Wazee
Sebleni yaliyopo Unguja.
Alitaja
vituo vingine vilivyopo mikoani vilivyopata zawadi hiyo kuwa ni kituo
cha The Village of Home cha Dodoma, kituo cha Moyo Mmoja cha Bagamoyo
mkoani Pwani, kituo cha watoto cha Tosamaganga kilichopo mkoani Iringa
na Mahabusu ya Watoto Arusha na Tanga.
No comments:
Post a Comment