Chama cha NCCR mageuzi jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro kimelaani
vikali kitendo cha madiwani wa chama cha Demokrasia na maendeleo chadema
kukata kumuunga mkono mgombea ubunge jimbo la Vunjo ambaye pia ni
mwenyekiti mwenza wa vyama vinavyounda katiba ya wananchi UKAWA Bw.James
Mbatia kwa tuhuma za kusimamisha wagombea madiwani kila kata.
Akitoa taarifa kwa waandishin wa habari katibu mwenezi wa chama cha
NCCR Mageuzi jimbo la Vunjo Bw.Stanley Temba amesema kitendo
kinachofanywa na madiwani wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA)
ni kinyume na makubaliano kwa kuwa lengo la muungano wa vyama hivyo ni
kupata ushindi kuanzian ngazi za chini hadi urais.
Amesema mgawanyiko huo utaasababisha wananchi kukosa imani na
viongozi wa vyama vinavyounda ukawa na kwamba ni vema madiwani hao
wakaacha hasira badala yake kukaa pamoja na kujadiliana ili kuondoa
kasoro zilizojitokeza badala ya kumsusia mgombea ubunge jimbo la Vunjo
kwa tiketi ya NCCR Bw.James Mbatia.
Naye mjumbe wa halimashauri kuu wa chama cha NCCR Mageuzi taifa
Bw.Hemed Msabaha amekiri kuwa chama hicho kimesimmisha wagombea udiwani
katika kata zote kwa madai kuwa viongozi wa chama hicho ndiyo
wanakubalika zaidi katika jamii ikilinganishwa na chama cha Demokrasia
na maendeleo Chadema.
Hata hivyo juhudu za kuwapata viongozi wa chama cha demokrasia na
maendeleo chadema mkoa wa kilimanjaro kuzungumzia sakata hilo
zinaendelea.chanzo Itv.co.tz
No comments:
Post a Comment