Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ameliambia
Baraza la Usalama la umoja huo kuwa muungano unaoongozwa na Saudi Arabia
katika mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Yemen unashambulia maeneo mengi
ya rais na yasiyo ya kijeshi.
Zeid Ra’ad Zeid Al-Hussein alisema jana katika kikao cha kwanza
cha wazi cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Yemen kwamba,
anafuatilia kwa wasiwasi mkubwa mashambulizi ya Saudi Arabia yanayolenga
miundombinu kama hospitali, shule na maeneo yenye makazi mengi ya raia
wa Yemen tangu nchi hiyo ianzishe mashambulizi ya anga miezi tisa
iliyopita. Ameongeza kuwa watu wapatao 6000 ambao nusu yao ni raia wa
kawaida, wameuawa katika mashambulizi ya Saudia huko Yemen.
Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ameliambia
Baraza la Usalama kwamba miongoni mwa matokeo mabaya ya mashambulizi ya
Saudia dhidi ya nchi iliyosambaratika ya Yemen ni kuwa maficho salama
kwa makundi yenye misimamo mikali kama lile la Daesh.
Mwezi Machi mwaka huu muungano unaoongozwa na Saudi Arabia ulianzisha
mashambulizi makali dhidi ya watu wa Yemen kwa kisingizio cha
kumrejesha madarakani rais aliyejiuzulu na kutoroka nchi Abd Rabbuh
Mansur Hadi-Chanzo irib
No comments:
Post a Comment